· Washiriki wanajisajili kwa mtandao,
Tigopesa
Usajili wa mbio za 18 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, Tigo
km 21 na Grand Malt Km 5 umeanza kwa kasi huku ukiwa juu kwa asilimia 30
ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana. Hili ni ongezeko la asilimia 10
ndani ya wiki moja.
Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa mbio hizo imeeleza kuwa
mwendendo ni mzuri na wamewataka washiriki kuchangamkia punguzo la bei
litakalodumu hadi mwezi Januari mwakani. Washiriki wanajisajili kwa kupitia www.kilimanjaromarathon.com
na kwa Tigopesa kwa kubonyeza *149*20#.
Mkurugenzi wa Mbio hizo nchini, John Bayo alisema kwa kupitia
taarifa hiyo kuwa kuna idadi maalumu ya washiriki inayotakiwa kwa mbio zote
tatu (Kilimanjaro Premium Lager Km 42, Tigo km 21 na Grand Malt Km 5) ili
kuhakikisha kuw ambio hizo zinaendana na viwango vya Shirikisho la Kimataifa la
Riadha (IAAF) ili kuhakikisha usalama unazingatiwa.
Kwa mujibu wa Bw. Bayo, hii pia itahakikisha washiriki wanafurahia
mbio hizo bila ya msongamano na pia kutoa nafasi kwa waandaaji waweze kutoa
huduma zinazotakiwa katika njia ya mashindano na sehemu ya kumalizia pia.
Kuhusu punguzo la bei, waandaaji hao pia
walitoa wito kwa washiriki wachangamkie utaratibu huo ambao ulianza Oktoba Mosi
2019 hadi Januari 14 , 2020. Kwa raia wa Tanzania na wale kutoka nchi za Afrika
Mashariki watalipa Tsh 15,000 kwa mbio za Km 42 na 21 na Tsh 5000 kwa km 5
lakini kuanzia Januari 15, 2020 hadi Februari 16, 2020 washiriki
watakaojisajili watalipa Tsh 20,000 kwa km 42 na 21 na Tsh 5000 kwa km 5.
Kwa wageni wakazi au wenye vibali vya
kuishi na kufanya kazi na wale wa nchi za SADC watalipa USD 35 kwa km 42 na 21
na USD 5 kwa km 5 kuanzia Octoba 1, 2019 hadi Januari 14, 2020 lakini kuanzia
Januari 15, 2020 hadi Februari 16, 2020 wanaojisajili watalipa USD 45 kwa km 42
na 21 na USD 5 kwa km 5.
Washiriki wa kimataifa watalipa USD 70 kwa
km 42 na 21 na USD 5 kwa km 5 kuanzia Oktoba 1, 2019 hadi Januari 14, 2020 na
kuanzia Januari 15 hadi Februari 16, 2020 watalipa USD 85 kwa km 42 na Km 21 na
USD 5 kwa km 5.
Kwa mujibu wa waandaaji hao, usajili
utafungwa rasmi saa sita usiku Februari 16, 2020 au pale ambapo idadi
inayotakiwa itatimia.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na
wawakilishi kutoka Chama Cha Riadha Tanzania, Baraza la Michezo Tanzania, Bodi
ya Utalii Tannzania na wadau wengine wa riadha.
Washiriki
pia walikumbushwa kuhusu vituo vya kuchukulia namba zao za ushiriki ambapo kwa
Dar es Sallaam ni Mlimani City kuanzia February 22-23, 2020, Arusha ni Hoteli
ya Kibo Palace kuanzia Februari 25-26 na Moshi ni Hoteli ya Keys kuanzia
Februari 27-28. “Washiriki watatakiwa kujitambulisha na kuthibitisha kuwa
wameshalipia kabla ya kukabidhiwa namba zao,” ilisema taarifa ya waandaaji.
Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2020 ni Kilimanjaro
Premium lager, Tigo, Grand Malt Kilimanjaro Water, TPC Limited, Simba Cement,
Barclays Bank na watoa
huduma rasmi ni Kibo Palace
Hotel, Keys Hotel, GardaWorld Security, Precision Air na CMC Automobiles.
Mashindano ya Kilimanjaro Marathon
yanayoandaliwa na Wild Frontiers na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive
Solutions, yanatarajiwa kufanyika Machi 1, 2020 katika Chuo Kikuu cha
Ushirika Moshi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇