LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 29, 2019

TANZANIA KUPIGA VITA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WA BINAADAMU



Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Zanzibar wamefanya majadiliano ya kupiga vita Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.

Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Ajira Ali Suleiman Ameir wakati wa Majadiliano kuhusu mipango mikakati yalifanyika huko katika Ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizini kati ya Shirika la IOM na Watendaji wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Zanzibar.

Majadiliano hayo ya Pamoja ni moja ya shughuli zitakazotekelezwa na IOM kwa mwaka huu wa miradi 2019/2020 ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mpango huo chini ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa Zanzibar (Zanzibar Joint Programme) kuhusu Msaada wa Maendeleo (United Nations Assistance Development Plan II 2016 -2021).

Mpango huo wa utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto 2017-2022 Zanzibar, utasaidia Kutoa mapendekezo ya tafiti iliyofanywa Zanzibar na Shirika la IOM juu ya Unyanyasaji Kiuchumi ikihusisha Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

Kati mipango hiyo ni Kukuza uelewa wa jamii juu ya dhana na aina za Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto, Utambuzi wa wahanga, Vyanzo na Madhara yake, Juhudi za Serikali na wadau katika utokomezaji wa udhalilishaji huo.

Pia Mjadala huo ulihusisha Nafasi ya viongozi katika jamii juu ya utokomezaji wa ukatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto pamoja na biashara haramu ya usafirishaji wa Binaadamu.

Hata hivyo washiriki wa kikao hicho walipendekeza Kuimarishwa ushirikiano wa wadau katika jamii juu ya juhudi za kutokomeza, ulinzi wa pamoja na kuongeza mwitikio wa huduma kwa wahanga wa Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu .

Majadiliano hayo ya siku mbili yalihusisha jumla ya washiriki 28 kutoka katika jamii, Viongozi wa Shehia, Mtaa, Viongozi wa Dini, Walimu wa Skuli za Msingi na Sekondari na Maafisa Ustawi wa Jamii .
Mkurugenzi wa Ajira  Ali Suleiman Ameir (katikati),akitoa maelezo kuhusiana na mikakati ya biashara haramu ya binaadamu  ( kushoto)  Msaidizi wa Programu ya Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM)  Enna Lutengano  na  Afisa  mipango Msaidizi  wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Zanzibar  Sarah Abdallah, huko katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizini.
 Washiriki wa majadiliano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakimsikiliza Mkurugenzi wa Ajira  Ali Suleiman Ameir huko katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages