RAIS
Dk. John Magufuli amewataka wakulima wote nchini kuuza mazao yao kwa bei
wanayotaka na kwamba Serikali haitapanga bei na badala yake jukumu hilo
libaki kwa mkulima mwenyewe.
Dk.Magufuli
ametoa kauli hiyo leo Novemba 20, mwaka 2019 akiwa katika eneo la
Dumila mkoani Morogoro.Rais alisimama kuzungumza na wananchi hao akiwa
njiani kuelekea mkoani Dodoma kikazi.
Akiwa
na wananchi hao, Rais Magufuli amekumbusha kuwa mvua zimeanza kunyesha,
hivyo watu wajihusishe na kilimo huku akieleza kuwa kuna watu
wanalalamika kupanda kwa bei ya mahindi lakini ifahamike Serikali
haitapanga bei.
Amesema mkulima mwenyewe ndio ataamua anataka kuuza bei gani kulingana na mahitaji ya soko kwa wakati husika.
"Nataka
Mkoa wa Morogoro uwe kinara katika kuzalisha mazao.Serikali
ninayoingoza katika kipindi changu sitapanga bei ya vyakula, wakati
mkulima analima hakuna anayempangia bei, hivyo anapouza mazao yaake
aachwe aamue anataka kuuza bei gani mazao yake,"amesema Rais Magufuli.
Ameongeza
hata kama mkulima ataamua kuuza debe moja la mahindi kwa Sh.milioni
moja sawa tu auze. "Hakuna kumpangia bei, wanaotaka bei nafuu wakalime
wao."
Amefafanua
ni kama ilivyo kwa mfugaji, anapouza ng'ombe huangalia bei ya soko ,
kama bei ya ng'ombe itakuwa juu atauza kwa bei ya juu, hivyo wakulima
nao waachwe wapange bei wenyewe."Soko liachwe liamue bei na sio
kupangiwa na Serikali."
Amesisitiza
watu waache kulalamika mahindi yamekuwa juu na hiki ndio kipindi cha
wakulima kunufaika na kilimo chao."Hata anayekuwa ofisini bado anaweza
kulima kwa kutumia fedha zake kumtuma mtu amlimie badala ya kulalamika
tu."
Rais
Magufuli amesema kwa sasa soko la mahindi na mazao mengine ni nzuri na
kuongeza nchi nyingi zinahitaji kununua mazao kutoka kwa wakulima wa
Tanzania, hivyo ni wakati wao kutajirika.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇