LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 20, 2019

EAC IMEZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 TANGU KUASISIWA MWAKA 1999


Na Ahmed Mahmoud Arusha

Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) jana imezindua rasmi maadhimisho ya miaka 20 tokea kuasisiwa upya kwa Jumuiya hiyo mwaka 1999 baada ya kuvunjika kw Jumuiya hiyo mwaka 1977

Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Balozi Liberatus Mfumukeko na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhandisi Steven Mlote Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha

Wakati wa Uzinduzi huo balozi Mfumukeko alitaja mafanikio yaliyopatikana katika Jumuiya hiyo katika Kipindi cha miaka 20 tangu kuasisiwa upya

Alisema mafanikio hayo ni ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, reli, miradi ya nishati (Umeme), miradi ya kujenga uwezo na usimamizi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Pia miradi ya kukabili na kujenga uwezo ili kuhimili mabadiliko katika nchi za EAC na pia miradi ya kuziba pengo kati ya Sera na Utendaji.Alieleza Balozi Mfumukeko

Katibu Mkuu huyo wa EAC alisema mafanikio hayo yametokana na ufadhili aidha wa misaada kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) k wa mikopo nafuu ama kama misaada ya Jumuiya hiyo

Alitaja miradi mingine ya miundo mbinu ni mradi wa upembuzi yakinifu na ujenzi wa mradi wa barabara ya Nyakanazi-Kasulu-Rumange hadi Bujumbura

Pia EAC inatekeleza mradi kwa ufadhili wa AfDB kupitia nchi wanachama za EAC wa barabara ya Lusahunga-Rusumo-Kayonza,Masaka-Mutukula-Kyaka hadi Rugen

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo alisema Mkoa wa Arusha ni moja ya Mikoa iliyonufaika zaidi na miradi iliyotekelezwa na EAC kupitia ufadhili wa AfDB

Alitaja barabara hizo kuwa ni barabara ya Arusha hadi Namanga, Sakina hadi Tengeru, Barabara ya Bye Pass ya Kutoka Ngaramtoni hadi Usa River

Mafanikio mengine ya Jumuiya hiyo ni utekelezaji wa miradi ya Kilimo na Viwanda katika nchi wanachama za EAC miradi ambayo inatekelezwa kwa msada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Alieleza Katibu Mkuu huyo wa EAC

Alisema Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo na Viwanda ni mambo ya muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Watu wan chi za Afrika ya Mashariki

‘Uchumi wa nchi hizi za EAC unategemea sekta ya Kilimo na Viwanda sekta ambazo ndizo mhimuli na nguzo kuu ya Uchumi wa Watu wake unaochangia asilimia 80 hadi 90 ya idadi ya watu waliomo katika nchi hizi’ Alisisitiza Balozi Mfumukeko

Alisema ‘Mafanikio katika kilimo ni muhimu kwa ajili ya kuwainua wananchi kuondokana na hali ya Umaskini .Pia Sekta hii inaajiri zaidi ya asilimia 80 ya wananchi kwani wengi wa wananchi hawa wanaishi maeneo ya Vijijini hivyo sekta hii inasaidia kuboresha Maisha ya wananchi wa mijini na Vijijini’

Hata hivyo Katibu Mkuu hali ya uchumi katika nchi hizi bado ulikuwa dhaifu hivyo ushirikiano wa mataifa haya utasaidia zaidi kujenga uchumi wa wananchi wa EAC

Alisisitiza kwamba’ watu mkiwa kitu kimoja utaimarisha zaidi nguvu katika kujenga uchumi imara na hivyo kuinua pato la nchi wanachama za EAC ambapo kwa sasa pato la nchi hii ni GDP 150’

Aidha alisema maendeleo ya mataifa yote duniani hata yale yaliyopiga hatua katika ukuaji wa uchumi wan chi hizo yanategemea zaidi ushiriki wa sekta binafsi

Katika kutekeleza programu mbalimbali mbali na sekta za miundo mbinu na nishati EAC imefanikiwa katika kutekeleza miradi ya elimu na afya kwa ufadhili wa benki hiyo

Pia ametaja mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 20 ya EAC ni kuanzishwa kwa mtangamano wa Soko la Pamoja, Ushuru wa Forodha pamoja na kuondoa Vikwazo mbalimbali vya kibiashara na Uingiaji wa watu kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine na pia kuondoa Vikwazo vya Visa

Kwa lengo la kuharakisha na kukuza biashara katika nchi wanachama za EAC pamoja na kupitisha sharia ya kuwa na sarafu moja EAC pia imeanzisha tume ya takwimu kwa nchi wanachama .Alisisitiza Katibu Mkuu

Aidha alifafanua kwmaba mafanikio mengine ni pamoja na kuwa na Shirikisho moja la Kisiasa na hadi sasa mchakato wa Katiba umezinduliwa mjini Kampala Uganda Novemba 18 na Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museven

Pia EAC imefanikiwa kushurikiana katika sekta ya afya kwa kuwa na maabara zinazotembea katika nchi wanachama ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ukiwemo ugonjwa hatari wa EBOLA

Hata hivyo Katibu Mkuu Mfumukeko alisema Mkutano wa Wakuu wan chi wanachama za EAC ambao ulikuwa ufanyike Novemba 30 mwaka huu 2019 hautafanyika nabadala yake mkutano huo utafanyika kati ya Januari na February mwakani 2020

Alisema ili mkutano wa wakuu wan chi ufanyike ni lazima Wakuu wan chi zote wanachama wahudhurie.Hata hivyo hakuweza kuelezea kwa kina Sababu zilizofanya mkutano huo kuahirishwa

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages