Muonekano
wa mradi wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Jijini Dodoma
unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB kwa kushirikiana na
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).
Kamishna
Msaidizi wa masuala ya Nishati ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati,
Mhandisi Innocent Luoga akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya AfDB, Bw. Amos Cheptoo (kushoto), katika chumba cha mitambo ya
kupozea umeme katika mradi wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Jijini
Dodoma.
Mratibu
wa mradi wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Jijini Dodoma, Mhandisi
Peter Kigandye (wa kwanza kushoto), akieleza utekelezaji wa mradi wa
Kituo cha Umeme cha Zuzu ambapo unatarajia kukamilika Februari, 2020,
wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), Bw. Amos Cheptoo (kushoto) ya kukagua mradi huo Jijini Dodoma.(Picha na Peter Haule, WFM, Dodoma)
Na Peter Haule, WFN, Dodoma
Benki
ya Maendeleo ya Afrika – AfDB imeridhishwa na kasi ya maendeleo ya mradi
wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kinachofadhiliwa na Benki hiyo kwa
kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan- JICA.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya AfDB, Bw. Amos Cheptoo,
alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Kituo hicho kilichopo katika
eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.
Bw.
Cheptoo alisema kuwa amejionea kazi nzuri inayofanywa na Mkandarasi ya
kuhakikisha mradi huo unakamilika Februari, 2020 na kutumika kikamilifu
katika kupoza na kusambaza umeme kwa manufaa ya Tanzania na nchi jirani.
Alisema
kuwa mradi huo utakua na tija zaidi baada ya kukamilika kwa mradi
mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere unaotarajia kuzalisha zaidi ya
Megawati 2000, hivyo kuifanya miundombinu ya kupoza umeme kutumika
kimailifu.
Mkurugenzi
huyo wa AfDB alisema umeme ndio nyenzo muhimu katika ukuzaji wa
uchumi na uendelezaji wa viwanda katika nchi za Afrika, kukamilika kwa
miradi ya umeme kutasaidia uwepo wa umeme wa kutosha hasa katika nchi za
Afrika mashariki na kusini mwa Afrika.
Serikali
ya Tanzania imechukua hatua nzuri za kuboresha miundombinu wezeshi ya
uzalishaji hasa Dodoma ambapo ndio Makao Makuu ya nchi.
Kwa
upande wake mratibu wa mradi huo Mhandisi Peter Kigandye alisema kuwa,
mradi huo utakuwa na uwezo wa kushusha umeme kwa Kilovoti 400 na kupoza
umeme wenye uwezo wa takribani megawati 400 kisha kusambaza umeme katika
maeneo mbalimbali mkoani Dodoma.
Gharama
ya mradi huo unajumuisha mradi mwingine uliopo Singida na gharama zake
ni dola za Marekani milioni 53 ambazo zimetolewa kwa ushirikiano wa
Serikali ya Tanzania, Benki ya AfDB na Shirika la JICA ambapo Kituo cha
Kupozea Umeme cha Zuzu kinagharimu takribani dola za Marekani milioni
22.
Aidha
Kamishna Msaidizi wa masuala ya Nishati ya Umeme kutoka Wizara ya
Nishati Mhandisi Innocent Luoga, ameishukuru Benki ya AfDB kwa kusaidia
uboreshaji wa miundombinu hasa ya umeme kwa kuwa miradi hiyo
itakapokamilika, utazinufaisha pia nchi za Zambia, Botswana na hata
Afrika ya Kusini, kupitia mtandao wa umeme wa kusini
Amewataka
wawekezaji walio na nia ya kuwekeza Dodoma kutumia fursa ya upatikanaji
wa umeme wa uhakika kuwekeza hasa katika viwanda vikubwa na vidogo kwa
kuwa mazingira ya uwekezaji yapo vizuri.
Mhandisi
Luoga ameiomba Benki ya AfDB kusaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya
usambazaji zaidi wa umeme katika Mkoa wa Dodoma na viunga vyake ili
kuchochea ukuaji wa uchumi na kulifanya jiji kuwa na hadhi stahiki.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇