Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha
Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam leo, ambao ni Mdhibiti
na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali, Katibu Tawala, Balozi, Kamishna
wa kazi katika ofisi ya Waziri Mkuu, na Majaji 12 wa mahakama kuu pamoja
na Mwenyekiti, na makamu mwenyekiti na Makamishna watano wa Tume ya
Haki za binadamu na utawala bora.
Akizungumza
na viongozi hao wateule, Rais Magufuli amesema kuwa walioteuliwa
wasidhani kuwa hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, Pia amewashauri
majaji wakafanye kazi kwa haki bila kumuonea Mtu, kwani hukumu hutolewa
na Mungu tu, ila kwa hapa duniani tunao Majaji.
"Kuna
watu ukiwateua wanadhani hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, wewe (CAG)
nilipokutoa toka kuwa Mkurugenzi wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania)
kwenda kuwa Katibu Tawala mkoa hukusema neno na ulikuwa mtulivu ,wapo
wengine ukiwatoa wanasema maneno maneno, wakati huo unapowateua huwa
hawasemi" Amesema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli amemuasa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutokuwaonea watu
pale anapopewa maagizo na mihimili mingine kama Bunge na Mahakama,
akatekeleze majukumu yake kwani yeye ni mtumishi na asibishane.
"Najua
CAG una 'Qualification' nzuri tu na huwa hatufanyi makosa tunapoteua,
form four ulitoka na divison one, form six ukatoka na division one hii
ni kuonesha wewe ni kipanga sio kilaza, 'Degree' ya sheria unayo,
ukachukua na masters, umefanya kazi sehemu nyingi tu" Amesema Rais
Magufuli.
Rais
Dkt John Pombe Magufuli leo Novemba 4,2019 amemuapisha Charles
Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
kufuatia uteuzi alioufanya hapo jana. Hafla ya kumuapisha Kichere ambaye
kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe pamoja na
viongozi wengine, imefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇