Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongozana jana na
viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Uyui kutoka Bwawa la Tura wilayani Uyui
ambapo ametoa milioni 300 kwa ajili ya kuanza ujenzi mradi wa
usambazaji maji katika eneo hilo.
Mbunge
wa Jimbo la Igalula Mussa Ntimizi akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Maji
Profesa Makame Mbarawa(mwenye kofia) jana wakati kiongozi wakati
alipokuwa na ziara ya kukagua Bwawa la Tura wilayani Uyui ili kuona
jinsi ya kujenga mradi wa kusambaza maji
*************************************
SERIKALI
imeahidi kutoa milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa usambazaji
wa maji kwa wananchi kutoka chanzo cha maji cha Tura wilayani Uyui ili
kuwaondolea kero ya upatikanaji wa maji ya uhakika ya muda mrefu kwa
wakazi wa eneo hilo.
Fedha hizo ni sehemu zitakazotumika katika kukamilisha mradi huo ndani ya kipindi cha miezi mitatu.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati wa
ziara yake Wilayani Uyui Mkoani Tabora kwa ajili ya kutatua kero za maji
kwa wananchi wa eneo hilo.
Alisema
kukamilika kwa chanzo hicho cha maji kitasaidia kuzalisha lita zaidi ya
milioni 2.7 na kuwahudumia wakazi zaidi ya 11,000 na hivyo kuwaondolea
usumbufu wa kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Alisema
kuwa Serikali haiwezi kuona wananchi wanateseka kutafuta maji kwa
umbali mrefu huku kukikwa na chanzo cha maji kizuri ambacho hakitumiki.
Waziri
huyo alisema mradi huo utakuwa na hatua tatu ambazo ni ujenzi wa kituo
cha kutoa maji kwenye bwawa na kusafisha maji, hatua ya pili ni ujenzi
wa tenki la upokeaji wa maji na hatua ya mwisho ni ujenzi wa
miundombinu ya usambazaji wa maji kwa wananchi.
Naye
Mbunge wa Jimbo Igalula Mussa Ntimizi alisema kuwa licha ya bwawa hilo
kumilikiwa na Shirika la Reli Tanzania(TRL) wamekubaliwa lianze kutumika
kutatua kero ya maji kwa wananchi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇