SERIKALI
imeamua kupeleka maji katika Kata ya Kigwa wilayani Uyui kupitia mradi
wa ujenzi wa bomba la maji kutoka Ziwa Victoria kwa gharama isiyopungua
shilingi bilioni 10.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa baada ya
kusikia kilio cha wakazi wa Kigwa cha tatizo la maji akiwa katika ziara
ya kusikiliza kero za wananchi.
Alisema
kuwa eneo hilo hakuna mto wala bwawa na ndio maana katika kata hiyo
kuna tatizo kubwa la maji na ndio maana Serikali imesikia kilio chao na
kuamua kutatua tatizo la wananchi hayo.
Waziri
huyo alisema kama Serikali imeweza kutoa maji kutoka Ziwa Victoria
haiwezekani kushindwa kupeleka maji kwa wakazi wa Kigwa ambao wako
umbali wa Kilometa 29 kutoka bomba kuu.
Profesa Mbarawa amesema mradi huo huo ukikamilika utasaidia kuwanufaisha vijiji 16 vya Jimbo la Igalula.
Alisema
utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza Mwezi Desemba mwaka huu na
kuongeza kuwa utekelezaji wa ujenzi wake utawahusisha vijana wa Kigwa,
Kwa
upande wa Mbunge wa Jimbo la Igalula Mussa Ntimizi aliishukuru Serikali
kwa uamuzi wake wa kuchukua maji kutoka mradi wa bomba la Ziwa Victoria
na kuwapelekea baadhi ya wakazi wa jimbo hilo ambalo lilikuwa
limesaulika katika mradi wa kwanza wa kuleta maji mkoani Tabora.
Alisema
hatua hiyo na ile ya kutekeleza mradi wa Tura itasaidi kuwatua ndoo
wanawake wa Kigwa kama walivyoaahidi kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM yam
waka 2015
Naye
Mkazi wa Kigwa Dotto Mrisho alisema kuwa 2010 walijengewa tenki la maji
ambapo yalitoka siku alipofika Waziri Mkuu wakati ule Mizengo Pinda
lakini baada ya kuondoka hakuna maji tena toka siku ile hadi leo.
Alisema
kitendo kile kiliwavunja moyo na kuona kila anapokuja kiongozi
anapowaambia kuwa wataletewa maji wanajua kuwa wanadanganywa.
Mrisho alisema kuwa anaamini juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano itawasaidia kuwaondolea kero ya maji katika eneo lao la Kigwa.
Semeni
Misana alisema tatizo la maji katika eneo hilo ni tatizo kubwa jambo
linalowafanya waamuke usiku sana kutafuta maji ambao wakati mwingine
wanakabiliwa na matatizo mengi ikiwemo kukataliwa na wenye visima.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇