Bonheur Malenga,
Mwanafunzi wa Chuo kikuu, alijikuta njia panda siku moja mwezi uliopita
akijiuliza kama anunue kifurushi cha intaneti au la.
''Nilikuwa nina njaa na sikujua kama ninunue chakula au kifurushi cha intaneti cha saa 24,'' aliiambia BBC.Mwanafunzi huyo mwenye miaka 27 anayesoma masomo ya uhandisi , huwategemea wazazi wake kwa fedha za kujikimu akiwa chuoni- lakini amekuwa akifanya matumizi ya zaidi ya kawaida kwa kuwa amekuwa akitumia mtandao kufanya utafiti wake kwa kuwa alikuwa mwaka wa mwisho wa masomo.
Anaishi Kinshasa, Mji mkuu wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambapo 26% ya wastani wa kipato hutumika na watumiaji wa simu kupata huduma za intaneti-njia rahisi za kupata mtandao wa intaneti hapa.
''Niliwaza kuwa kukaa na njaa kwa siku moja na usiku hakutaniua. hivyo, nilinunua kifurushi na nikalala tumbo langu likiwa tupu,'' alisema.
Bwana Malenga anasema hata marafiki zake wengi wanakabiliwa na hali hiyohiyo.
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo ni nchi iliyowekwa katika kundi ambalo ni ghali sana kupata huduma za mtandao duniani, kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2019 kuhusu upatikanaji wa huduma za mitandao uliofanywa na taasisi ya Alliance for Affordable Internet.
Taasisi hiyo inasema kuwa gharama ndogo ni 2% au chini ya wastani huo wa kipato cha mwezi katika GB 1.
'Viatu vyangu vilichukuliwa na msimamizi wa cybercafé
Katika eneo la upande wa pili wa nchi yangu zaidi ya umbali wa kilometa 2,000 mashariki mwa Kinshasa, Eric Kasinga anakumbuka vipindi vya udhalilishaji alivyovipitia miaka michache iliyopita.
Kama ilivyo kwa vijana wadogo waishio mji wa Bukavu, alilazimika kwenda kwenye vibanda vinavyotoa huduma ya intaneti. Alikuwa akijisajili masomo ya juu katika vyuo vinavyoheshimika nchini Uholanzi.
Kasi ya inteneti ilikua ndogo sana, hata mchakato wa maombi ya chuo ulichukua saa tatu badala ya moja,'' alisema
Lakini alikuwa na pesa ya kulipia saa moja pekee.
Alieleza hali ilivyokuwa kwa msimamizi wa eneo hilo, akiwa na matumaini kuwa atamruhusu ampelekee fedha baadae.
Hata hivyo meneja huyo alianza kupiga kelele na kumtamkia maneno ya matusi: akisema ''intaneti si ya watu masikini.''
Kufidia hicho, meneja alimvua viatu vipya alivyokuwa amevaa bwana Kasinga, akitaka atembee pekupeku kuelekea nyumbani.
''Nilisikia aibu kweli,'' anasema.
Kasinga, ambaye sasa anafanya kazi kwenye taasisi ya uhifadhi, hakuweza tena kufuatilia maombi yake ya chuo kikuu. Alijaribu kufuatili viatu vyake lakini meneja tayari alikwishaviuza viatu.
DR Congo ni nchi ya nne kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, theluthi mbili ya idadi ya watu mashariki wa bara la Ulaya na ni nchi yenye utajiri mkubwa wa madini yanayotumika kutengeneza simu.
Lakini wananchi wake wanapata wakati mgumu kupata huduma za msingi kama vile za kiafya, maji safi ya kunywa na umeme.
Kwao, kupata huduma za intaneti, ilielezwa na ofisi ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa kuwa, inatazamwa kama jambo la anasa.
Mamlaka ya mawasiliano nchini Drc inakisia kuwa 17% ya wananchi wanapata huduma za intaneti.
Ripoti nyingine ya hivi karibuni pia imeonyesha tofauti ya matumizi ya intaneti kati ya wanaume na wanawake. Zaidi ya 33.8% ya wanaume tofauti ya 22.6% ya wanawake Afrika wana huduma za intaneti ilisema Jumuia ya kimataifa ya mawasiliano.
Profesa Kodjo Ndukuma, mtaalamu wa masuala ya haki za digitali mjini Kinshasa amesema kuna sababu kuu tatu kuhusu uwepo wa gharama kubwa za intaneti.
1.Hakuna anayefahamu gharama za kweli za huduma
Gharama hutengenezwa unapofanya hesabu kwa misingi ya uwekezaji uliowekwa na kampuni ya mawasiliano, gharama za uendeshaji na idadi ya watumia huduma.'' anaeleza.
Mahesabu haya hufanywa kwa simu za sauti lakini hakuna kampuni ya mawasiliano imefanya hayo kwa data za intaneti, kumaanisha kuwa mdhibiti hawezi kufahamu ukweli kuhusu gharama.
Mapungufu hayo hutoa mwanya kwa makampuni kuweka gharama zozote wanazozitaka,'' anasema Profesa Kodjo
2. Kukosekana kwa ushindani
Idadi ya watumiaji na idadi ya makampuni ya mawasiliano yameendelea kushindwa kusonga mbele kwa miaka mingi.
''Idadi ndogo ya kampuni huamua kitu kimoja na hakuna wa kuwazuia,'' anasema profesa Kodjo.
Alitoa mfano wa mwaka 2016 wakati makampuni yote ya simu nchinI Drc, yalikubaliana kuongeza gharama za data kwa asilimia 500.
3. Kodi kubwa
''Makampuni ya simu hulipa kodi ambayo madhara yake wanaoumia ni watumiaji wa mwisho.'' anasema profesa.
- Unaweza pia kusoma
- Facebook yazitaka serikali ziwe na udhibiti wa kisheria
- Huduma ya intaneti yafungwa DR Congo siku moja baada ya uchaguzi
Kati ya mwezi Machi na Oktoba, kundi hilo liliandaa maandamano 11 nchi nzima kushinikiza kushushwa kwa gharama za intaneti.
''Mamlaka ya mawasiliano ilituambia kwenye mkutano kuwa kuna ukomo wa kisheria kuhusu mipaka ya kuingilia shughuli za makampuni ya simu,'' alisema Bienvenu Matumo kutoka La Lucha.
''Bado tunataka serikali kufanya kitu badala ya kutazama tukiibiwa.''
Waziri wa teknolojia ya mawasiliano aliwaita wanachama wa La Luta, na makampuni ya simu kuja na suluhisho la mvutano huo-serikali yenyewe hairuhusiwi kisheria kuingilia kati.
Lakini mkutano wa kwanza ulishindwa kuja na njia mwaaka za kupunguza gharama au kuboresha huduma za intaneti.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇