Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema Serikali imemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mbolea nchini (TFC), pamoja na kumuagiza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya BAJUTA kuzirudisha haraka iwezekanavyo, fedha za umma kiasi cha Shilingi Bilioni 4.5
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mbolea nchini (TFC) Asimamishwa Kazi
Naibu Waziri Bashe ametoa kauli hiyo leo Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Chunya, Victor Mwambalaswa, lililokuwa likihoji nini hatma ya mbolea na viuatilifu vya zao la korosho, ambavyo licha ya Serikali kutoa pesa ni mwaka sasa umepita mbolea na viuatilifu hivyo bado viko bandarini.
Akijibu swali hilo Bashe amesema; “Ni kweli Serikali ilitoa pesa Bilioni 10 kwa ajili ya kuagiza viuatilifu hivyo na Serikali imemsimamisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TFC kama hatua ya awali kwa uzembe huu”.
“Nitumie nafasi hii ndani ya Bunge hili kuagiza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bajuta kurudisha Bilioni 4.5 alizopewa na tumeongea na TPA wamekubali kutuondolea gharama zote na sasa tuko katika hatua za mwisho kuvitoa viuatilifu hivyo kabla havijaharibika ili tuweze kuwagawia wakulima” Bashe.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇