"Finest Valor" Ujasiri wa Pekee" Simulizi ya Kuibuka kwa Rais John Pombe Magufuli.
KITABU
cha Mafanikio ya Rais Dr.John Pombe Magufuli, kuanzia mchakato wa
kumpata kama mgombea, kampeni ya Urais 2015, kuapishwa Novem Ba 5 2015,
sera na mipango yake.
Ujasiri
wa kusimamia rasilimali za nchi, kufufua shirika la ndege, kujenga
misingi ya uzalendo, sera ya mambo ya nje na kufanikiwa kupambana na
rushwa na ufisadi kwa kiwango cha juu.
Kitabu
hicho kimeandikwa na Novatus Joseph Igosha Mwanasheria Wizara ya katiba
na sheria na kinatarajiwa kuzinduliwa Disemba 2019.
Kimehaririwa na Spika mstaafu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa, kitabu hicho kwa sasa kimepitishwa katika kampuni ya Afrika kusini inaitwa Reach Publishers.
Kitabu
hicho kinalengo la kujenga uzalendo kwa kuonesha ujasiri wa serikali ya
Rais Magufuli katika kuwatumikia wananchi kwa kufanya maamuzi kijasiri
katika kusimamia rasilimali za nchi, kupambana na rushwa na ufisadi
kizalendo.
Ila pia kutambulisha upekee wa serikali hii katika kujenga uchumi wa kati na wa viwanda kwa siku zijazo.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇