Na Shushu Joel
MBUNGE
wa Jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete ameitaka serikali kuwatumia
wazee wa maeneo husika ili kuondoa migogoro ya mipaka baina ya Kijiji na
Kijiji au ile ya kata kwani kwao wameishi maeneo hayo kwa kipindi
kirefu.
Rai
hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa jimbo la chalinze
ambapo mbunge huyo alisisitiza kuwa endapo wazee wakipewa nafasi ya
kutatua migogoro hiyo itabaki kuwa ni historia.
Aliongeza
kuwa katika jimbo lake kuna changamoto ya uwepo kwa baadhi ya maeneo
kuwa na matatizo hayo hivyo amewashauri wataalamu wa idara ya ardhi
kuwatumia wazee wa maeneo husika kwani wanaweza wakawapa mwelekeo wa
kujua jinsi ya kumaliza changamoto hizo.
“Nimefanya
mikutano katika jimbo langu kwenye vijiji taklibani vyote hivyo mimi
kama mbunge nimeshauri kutumiwa kwa wazee ili kutatua changamoto
hiyo”Alisema Kikwete.
Aidha
aliongeza kuwa kitu kingine ambacho kimekuwa kikiwachanganya wananchi ni
maamuzi yanayofanywa na wataalam katika utatuzi wa migogoro hiyo kwa
wao kwenda kwenye maeneo na kuwahusisha watu ambao si sahihi.
Kwa
upande wake mzee Said Lufunga (79) amempongeza mbunge kwa kutambu
changamoto za mipaka ambazo zimekuwa ni kero kubwa katika jamii.“Ukimuona nyani kazeeka amekwepa mishale mingi hivyo aminini wazee ni kimbilio la matatizo yote” Alisema Lufunga.
Naye
Bi, Amina Ramadhani(76) amesema kuwa migogoro inatengenezwa na wataalam
kutokana na kutotaka kusikiliza wazawa kwani wao wamekuwa wakitumia
vifaa vya kisasa tu.Hivyo amemuomba mbunge Kikwete kuendelea kulipigia kelele Jambo hili uenda mwafaka ukapatikana.
“Wazee
kwa kushirikiana na viongozi wa dini wanaweza wakawa suluhiaho la hili
Jambo katika halmashauri yetu ya chalinze ” Alisema.
Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akizungunza na baadhi ya wazee jimboni humo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇