LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2019

ZAIDI YA WAFANYAZIARA MILIONI 17 WASHIRIKI KATIKA ARUBAINI YA IMAM HUSSIN (AS) YA MWAKA HUU

Gavana wa mkoa wa Karbala nchini Iraq ametangaza kuwa, idadi ya mazuwari walioshiriki kwenye maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein (as) mwaka huu imepindukia milioni 17.
Nassif Jassem al-Khattabi, ameyaeleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kubainisha kuwa, wafanyaziara walioshiriki katika Arubaini ya Imam Hussein (as) mwaka huu ni wengi zaidi kuliko mwaka uliopita na akaongeza kwamba, mipango yote iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapokea na kuwahudumia mazuwari wa Arubaini, ikiwemo utoaji wa huduma za usafiri na afya, ilitekelezwa vizuri sana.
Naye Ali al-Hamdani, kamanda wa operesheni iliyopewa jina la Al-Furatul-Awsa't, ya ushirikishaji wananchi amesema, mkakati wa usalama kwa ajili ya Arubaini umetekelezwa kwa mafanikio na akabainisha kwamba; mpango huo wa usalama umetekelezwa kwa uratibu na ushirikiano wa vikosi vyote vya usalama katika sura ya kikosi kimoja.
Tarehe 20 Mfunguo Tano Safar mwaka 1440 Hijria iliyosadifiana na tarehe 19 Oktoba 2019 Miladia ilifanyika Arubaini ya Imam Hussein (as) na wafuasi watiifu na waaminifu waliouawa shahidi pamoja na mtukufu huyo katika jangwa la Karbala mwaka 61 Hijria.
Kila mwaka mamilioni ya wafanyaziara kutoka kila pembe ya dunia huelekea Karbala, Iraq kushiriki kwenye Arubaini ya Imam Hussein (as).../

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages