LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2019

MACHAR: SPLM-IO HAITASHIRIKI KATIKA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA SUDAN KUSINI

  • Riek Machar
Kiongozi wa kambi kuu ya upinzani nchini Sudan Kusini ameuambia ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuwa hatashiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa itakayoundwa mwezi ujao nchini humo.
Riek Machar amesema kuwa pande husika katika mgogoro wa Sudan Kusini zimeshindwa kufikia makubaliano juu ya jinsi ya kuliunganisha jeshi la nchi hiyo suala ambano ni sharti muhimu katika makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka jana; kwa msingi huo hakuna uwezekano wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
Matamshi hayo ya Machar yameondoa uwezekano wa kupatikana maendeleo katika mchakato wa kurejesha amani nchini Sudan Kusini.
Anesena: "SPLM-IO haitashiriki katika serikali hiyo kwa sababu haitaki kuitumbukiza nchi katika mgogoro."
Hata hivyo ujumbe wa Umoja wa Mataifa umesema kuwa matatizo yaliyoashiriwa na Riek Machar yanaweza kupatiwa ufumbuzi kabla ya tarehe 12 Novemba.
Riek Machar akisalimiana na ujumbe wa UN
Mwezi Mei mwaka huu pande mbili hasimu nchini Sudan Kusini zilitia saini makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika kipindi cha miezi sita ijayo na kuunda serikali ya mpito hadi kufikia tarehe 12 Septemba.
Sudan Kusini ilitumbukia katika vita vya ndani Disemba 2013 baada ya Rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar wa kabila la Nuer kwamba alihusika na jaribio la kuipindua serikali yake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages