LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 19, 2019

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI MIKE POMPEO NA WAZIRI MKUU WA ISRAEL BENJAMIN NETANYAHU WAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO

Pompeo- Netanyahu wazungumza
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Morgan Ortagus, ametoa taarifa kwamba mara baada ya mkutano wa siku ya Alhamisi jijini Ankara waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alikwenda Tel Aviv.

Pompeo alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Wawili hao walikutana mjini Jerusalem na kufanya mazungumzo yaliyohusu kuimarsha mahusiano ya mataifa hayo mawili.
Ortagus alibainisha pia katika mazungumzo ya wawili hao walijadiliana kuhusu suala la usalama wa kanda pamoja na yanayojiri kaskazini mwa Syria ikiwamo makubaliano baina ya Marekani na Uturuki.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages