LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 20, 2019

MOI WAANDAA MECHI YA HISANI

Taasisi ya Mifupa (MOI) imeandaa mechi ya hisani ili kuchanga fedha kwa ajili ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na wagonjwa waliotelekezwa na ndugu zao, Mechi hiyo ya kirafiki itazikutanisha timu machachari ya MOI na ile ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar. Mechi itafanyika siku ya kilele cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Watoto wenye Vichwa Vikubwa na Mgongo wazi tarehe 25 Oktoba 2019. Mechi itafanyika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, liingilio jukwaa kuu ni shilingi elfu tano na mzunguuko ni shilingi elfu tatu. ''Wananchi wote wanakaribishwa kushuhudia mechi safi kutoka kwa wataalam wa tiba mbalimbali. Lakini pia kuhudhuria kwao ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi ya MOI kutoa huduma bora kwa wahitaji''. Alisema Patrick Mvungi nahodha wa timu ya MOI ambao ndio waandaji wa mechi hiyo.   

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages