Serikali imesema ipo tayari kulipa Deni la shilingi Bilioni 13 kwa wakulima wa korosho Wilayani Tandahimba.
Hayo
ameyasema Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba wakati akijibu maswali na
kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Kijiji Cha Nachunyu
"Msema
kweli mpenzi wa Mungu,tulishindwa kuendelea kuwalipa kwakuwa fedha
ilituishia,lakini Sasa tumeshapata fedha baada ya kuuza korosho zetu
zote tan220,000 kwaiyo fedha tunayo tunauhakika wa kuwalipa
wakulima,"alisema Mgumbo
Alisema serikali inatarajia kulipa madeni kwa wakulima na vibarua Tanzania nzima shilingi Bilioni 89 ambazo zipo.
"Utaratibu
utafanyika katika malipo hayo lakini fedha kwa Sasa ipo,sababu tulikuwa
tunalipwa kwa malipwani yaani mzigo upakiwe kwenye meli ndipo malipo
yafuaate kwaiyo tumemaliza zoezi hilo ," alisema Mgumbo
Aidha alisema maghala yapo wazi tayari kwa kupokea mzigo mpya hivyo muda wowote wataanza kupokea korosho kutoka kwa wakulima
Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumbo na Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba akipata maelezo kutoka kwa mkulima Ahmad Ulenje
Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumbo akifafanua jambo wakati akijibu maswali na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Kijiji Cha Nachunyu
,kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba .
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇