Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda ameelekeza Watumishi wa
TAMISEMI wanaohusika na Miradi ya ujenzi wa Mifereji na Mito kupitia
DMDP kuhakikisha kabla ya October 10 mwaka huu miradi yote ya Ujenzi wa
Mifereji Wilaya ya Ilala iwe imeanza na endepo watakaidi atahitisha
maandamano ya wakazi wa Kata 5 kwenda Wizara ya TAMISEMI.
RC
Makonda ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea Mfereji wa Kisiwani
kata ya Buguruni ambao tangu mwezi May mwaka huu aliagiza ufanyiwe
maboresho kutokana na mfereji huo kuwa chanzo cha mafuriko kwenye makazi
ya watu lakini ameshangazwa kuona hadi leo anafika site anakuta hakuna
chochote kilichofanyika licha ya mkataba kusainiwa tokea mwezi wa Saba
mwaka huu.
Jambo
hilo lilimlazimu RC Makonda kumpigia simu Mratibu wa Miradi ya DMDP
Bwana Emmanuel Ndyamkana ambae alijitetea kuwa miradi hiyo inakwama
kutokana na wizara ya fedha kuchelewa kutoa fedha jambo ambalo RC
Makonda amesema ni uzembe.
Aidha
RC Makonda ameitaja baadhi ya Mifereji na Mito inayotakiwa kufanyiwa
maboresho ni pamoja Mfereji wa Tabata kanisa la Roman catholic, mfereji
wa Kiwalani na baadhi ya Mito yenye urefu wa Km 19 ambayo ujenzi wake
utagharimu takribani Shilingi Bilioni 32.
Pamoja
na hayo RC Makonda ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Machinjio mpya ya
Vingunguti na kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambapo amewataka NHC
kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇