Mbunge
wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimuonyesha kaimu meneja
wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi kwa namna gani daraja hilo
lipo hatarini kubomoka
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikagua moja ya madaraja ambavyo yamelalamikiwa kwa ubovu .
Mbunge
wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akipata maelezo kutoka kwa
kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi kwa namna
gani watatengeneza barabara hiyo ili ichochee maendeleo kwa wananchi
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
JUMLA
ya milioni mia tisa ishirini na moja zinatumika katika kutatua Tatizo la
barabara kuanzia Mkuta hadi Mpangatazara kwa kiwango cha changalawe
katika jimbo la Mufindi Kaskazini kwa lengo la kurahisisha shughuli za
kimaendeleo ambazo zimekuwa zikihusisha barabara hiyo.
Akizungumza
kwenye mikutano ya hadhara ya mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini
Mahmoud Mgimwa,kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi
alisema kuwa pesa tayari imepatika na tayari wameshawapata wakandarasi
ambao watatengeneza barabara hizo.
“Mheshimiwa
mbunge na wananchi wako mwezi huu wa kumi tunaanza kutengeneza barabara
hii ambayo imekuwa kimbilio la maendeleo kwa wananchi wa jimbo hili
hasa katika biashara ya usafirishaji wa zao la mbao ambalo ni chanzo
kikubwa cha mapato kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini” alisema
Mjohi
Mhandisi
Mjohi alisema kuwa barabara hiyo inayotengenezwa itapita katika vijiji
vya Ifwaji,Ifupira,Kidete,Ikanga,Ihanu,Ibwanzi,Lulanda,Isipii na Mpanga
Tazara kwasababu vijiji hivi vipo barabarani kabisa lakini vijiji zaidi
ya arobain vitanufaika na barabara hiyo kimaendeleo.
“Barabara
hii ikikamilika itahudumia zaidi ya vijiji arobaini ambavyo vipo
pembezoni au vinazungukwa kwa namna moja au nyingine na barabara hii
ambayo imegharimu mamilioni ya pesa ambazo zimetafutwa na mbunge wa
jimbo hili” alisema Mjohi
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa
aliwahakikishia wananchi kuwa barabara hiyo itatengenezwa kwa kuwa fedha
ametafuta na amewakabidhi kwa TARURA wilaya ya Mufindi na tayari
wameshapata wakandarasi wawili ambao watatengeneza barabara hiyo kwa
kiwango cha changalawe.
“Mimi
mbunge wanu nimeshafanya kazi yangu ya kutafuta fedha nimepata na
nimekabidhi kwa wataalam hivyo kazi iliyobakia ni kuhakikisha wataalum
wanasimamia vilivyo barabara hii ili ijengwe kulinga na gharama ambazo
zimetolewa” alisema Mgimwa
Mgimwa
mgimwa alisema kuwa barabara hiyo inaumhimu mkubwa kwenye biashara ya
zao la mbao kwa kuwa ndio baishara kuu inayofanyika katika barabara hiyo
na kuwakumbusha wananchi kuwa barabara hiyo ni yao na wanapaswa
kuisimamia.
Nao
wananchi waliendelea kumkubusha mbunge umuhimu wa barabara hiyo
kimaendeleo kwa kuwa wananchi wamekuwa wakiitumia katika shughuli za
kimaendeleo za kila siku.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇