LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2019

MICHUANO YA BASHUNGWA KARAGWE CUP YAHITIMISHWA


Baadhi ya wananchi na mashabiki wa michezo waliojitokeza kushuhudia fainali za Kombe la Bashungwa Karagwe Cup.
 Mkuu Wa Mkoa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti akiwasili katika viwanja vya Kayanga kuungana na maelfu ya wapenda soka katika Kilele cha Michuano ya Bashungwa Karagwe Cup, Pembeni ni Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheluka na Mwenyekiti Wa Ccm Karagwe Robinson Mutafungwa.
 Picha ya pamoja wamuzi pamoja na manahodha Wa Timu zilizotinga Fainali, Nyakahanga na Nyakabanga, ambapo mwamuzi Wa kati aliechezesha mchezo huo ni Ahmada Simba.
 Mgeni Rasmi Naibu Waziri Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu (MB) akiwa na Mwenyeji wake Innocent Bashungwa Waziri wa Viwanda na Biashara (MB) wakielekea uwanjani kukagua timu mapema kabla ya kuanza mchezo wa Fainali
 Mikakati ikiwekwa sawa ya kuwa na Mechi kati ya Karagwe Combine, na Bukoba Combine ambapo baada ya Wiki tatu kuanzia sasa Itapigwa mechi hiyo na Mshindi akiondoka na Milioni 2, na Milioni moja kwa atakaefungwa, hiyo ni kwa Mujibu wa Marco Gaguti RC - Kagera.
 Kinyuri nyuri cha Bashungwa, Mama Alaska akifuatilia mtanange, mbali na yote amemuunga mkono Mumewe kwa kutoa zawadi ya Shilingi Laki tano kwa mshindi wa kwanza na laki tano kwa mshindi wa pili.
 Mwali akiletwa uwanjani mapema kabla ya kuanza kwa kipindi cha pili cha mchezo wa fainali ya Bashungwa Karagwe Cup
 Kipa wa Nyakabanga akipangua mkwaju wa mwisho wa penati, kutoka kwa mchezaji wa Kayanga na kupelekea kuipa ushindi Timu yake kwa Kuibuka mshindi wa Tatu, Mchezo huo ulitangulia mapema kabla ya mchezo wa Fainali.
 Mgeni Rasmi Costantine Kanyasu Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Akikabidhi Zawadi kwa Mshindi wa Tatu, nahodha wa timu ya Nyakabanga, Kiasi cha Shilingi Laki Nne na Nusu na jezi seti moja.
 Mgeni Rasmi Costantine Kanyasu Naibu Waziri Maliasili na Utalii, akikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili, nahodha wa Timu ya Kamagambo Milioni moja Laki sita na Nusu na Seti moja ya Jezi
Mabingwa wa Mashindano ya Bashungwa Karagwe Cup 2019, Timu ya Kata Nyakahanga wakishangilia ushindi Mara baada ya kukabidhiwa Zawadi zaoAnaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV

Michuano ya Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Karagwe Innocent Ruga Bashungwa (Mb) ambae pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara imefikia tamati leo hii toka ilipoanza mwanzoni mwa mwezi Agost 2019 kwa timu ya Kata ya Nyakahanga kuchukua ubingwa huo katika msimu wa pili wa ligi hiyo, baada ya kuifunga timu ya Kata ya Kamagambo kwa penalti 3-2 Katika Uwanja mpya wa Bashungwa uliopo mjini Kayanga Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

Kilele cha mashindano hayo  kilitanguliwa na mchezo wa awali wa  mshindi wa tatu kwa kuzikutanisha Timu za kata ya Nyakabanga na Kayanga, ambapo Nyakabanga wameibuka kidedea kwa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Kata ya Kayanga baada ya Timu hizo kutoshana Nguvu kwa Dakika 90 za mchezo.

Mgeni rasmi katika mchezo wa Fainali hizo Constantine Kanyasa (Mb) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amesema amefurahishwa na Fainali hizo na huku akiduwazwa na umati wa mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo,  ikiwa ni ishara ya upendo mkubwa wa wananchi hao dhidi ya Mbunge wao pamoja na michezo kwa ujumla, licha ya mambo mengine Kanyasu amesisiitiza juu ya Vijana na wananchi kuendelea kutangaza Utalii kupitia michezo hususani hifadhi mbili za Burigi - Chato na Ibanda - Rumanyika zilizopo katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa.

Kwa upande wake Mwenyeji na muandaaji wa  mashindano hayo  Mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Luga Bashungwa, amewashukuru wote waliofanikisha mashindano hayo kubwa akizidi kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo amekuwa akimsaidia kwa kumuunga mkono, lakini pia kwa jinsi alivyoendelea kumuamini na kwamba hatomuangusha 
Huku akiongeza kuwa kupitia michezo ataendeleza mshikamano na mahusiano kati ya Vijana na Serikali, ikiwa pia michezo ni ajira, afya na Utalii.

Bingwa wa michuano hiyo Timu ya Nyakahanga wameibuka na Kitita cha Shilingi  amejipatia Tsh 2,500, 000/=, jezi seti 1 na Kombe, 
Mshindi wa pili amejipatia Tsh 1,650,000/= na jezi seti 1.
Mshindi wa tatu amejipatia Tsh 450,000/= na jezi seti 1.
Mshindi wa nne amejipatia Tsh 300,000/ na jezi seti 1, huku Zawadi hizo zikinogeshwa na Zawadi kutoka Kwa Mgeni rasmi Aliyeongeza Laki mbili Kwa Mshindi wa kwanza na pili, wakati Mke wa Waziri Bashungwa Mama Alaska akiongeza Milioni Moja katika Zawadi za washindi .Zawadi nyingine ni Timu yenye nidhamu imejipatia jezi seti 1, Zawadi nyingine zilikuwa za: 
Golikipa bora, Mfungaji bora na Mchezaji bora kila mmoja amejinyakulia Tsh 50,000/=

Kupitia mashindano hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti ametangaza mechi kati ya Bukoba combine na Karagwe Combine mchezo utakaochezwa wiki tatu zijazo na Mshindi atazawadiwa Milioni Mbili, na atakaeshindwa atapata kifuta jasho shilingi Milioni Moja.

Awali ligi hiyo ilishirikisha timu zote za kata  23 zilizopo Wilaya ya Karagwe huku kila timu ikipewa seti moja ya jezi na mpira mmoja kwa ajili ya michuano hiyo. Pia viongozi wengine waliohudhulia fainali hiyo ni Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheluka viongozi  wa Chama na Serikali
na watu Mashuhuri.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages