LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 22, 2019

MRADI WA KILIMO KUWAFIKIA WAKULIMA WA MIGOMBA BUKOBA




Na Lydia Lugakila Bukoba


Jumla ya Wakulima wapatao 5,000 wanatarajia kufikiwa na mradi wa kilimo bora cha migomba katika kata zilizopo kando kando ya ziwa ikimba katika Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera.

Hayo yamebainishwa leo oktoba 22, 2019 na Afisa Ugani  Deusdedit Rweyemamu anayesimamia eneo laziwa ikimba wakati alipotembelewa na wana mradi ambapo amesema   mradi huo ulianza februari mwaka huu na kwamba lengo kubwa la mradi huo kuongeza ubora katika zao la migomba na kuwa  Jumla ya Wakulima wapatao 5,000 wanatarajia kufikiwa na mradi wa kilimo bora cha migomba.

Rweyemamu amezitaja kata zenye mradi huo kuwa ni kata ya Izimbya , Rubale, Kaibanja, Kyamulaile, Ruhunga, Kikomero na Buterankuzi zilizopo mkoani hapa.

Aidha ameongeza kuwa  katika kata ya Buterankuzi  kuna  mashamba darasa 27, ambayo  husaidia wakulima kwenda kujifunza kilimo  bora cha migomba na kisha kwenda kuboresha mashamba yao.

Baadhi ya wakulima ambao wako katika mradi huo wamesema kabla ya mradi huo migomba yao ilikuwa inastawisha chane mbili za ndizi lakini kwa sasa kutokana na elimu waliyoipata tayari wameanza kustawisha migomba mizuri ambapo  wanatarajia itakuwa na chane kuazia kumi na kuendelea

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages