NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MAGARI
ya abiria kumi,yafanyayo safari zake Mbezi -Tumbi na Mbezi-Mlandizi
yamekamatwa na kupigwa faini ya sh.100,000 kutokana na kukiuka kosa la
kukatisha ruti.
Aidha
magari yafanyayo safari zake Bagamoyo -Tegeta Nyuki na Kisarawe
yametakiwa kutoza nauli zilizowekwa kisheria ili kuondoa malalamiko kwa
abiria.
Akielezea
kuhusu taarifa hiyo, ofisa mfawidhi SUMATRA,Mkoa wa Pwani ,Omary Ayubu
alisema, wanatekeleza maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Pwani baada kupokea
malalamiko na kuomba watatue tatizo la kukatisha ruti.
Alieleza , magari matatu yamekatisha ruti kutoka Mbezi – Tumbi ambayo yaligeuzia Njuweni na mengine saba yaligeuzia Kongowe.
Ayubu
alisema ,wataendelea kuwachukulia hatua kali madereva na wamiliki wa
magari hayo ili iwe fundisho kwa wengine ambapo mbali ya faini watapaswa
kuzingatia taratibu za leseni zao pasipo kugeuza njiani.
”
Zoezi hili ni endelevu ,hatuishii hapa ,licha ya mkuu wa mkoa kutoa
maelekezo lakini na sisi tumejipanga kushirikiana na jeshi la polisu
kupitia kikosi cha usalama barabarani.”
“Wamiliki
wajieleze kwa siku saba ,kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua kali ya
kufungiwa leseni au kufikishwa mahakamani.”Alibainisha Ayubu.
Akieleza
kuhusu magari ya abiria yanayokwenda Bagamoyo kupitia Baobao alisema,
wanaendelea kusisitiza wamiliki kuona umuhimu wa barabara hiyo.
Ayubu
alifafanua, nayo magari yanayofanya safari zake Makumbusho-Tegeta Nyuki
na njia ya kwenda Kisarawe waache kuzidisha nauli wafuate sheria na
nauli zilizopangwa bila kuwaumiza abiria.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇