LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 30, 2019

DKT. SHENI MGENI RASMI UZINGUZI MELI MPYA YA MAFUTA


Na Thabit Madai,Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Sherehe ya uzinduzi wa Meli ya MT. Ukombozi II siku ya Jumanne Octoba Mosi mwaka huu.

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa Waandishi wa habari na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Mustapha Aboud  Jumbe alisema kuwa Dk Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  Sherehe hizo za Uzinduzi wa meli hiyo mpya ya Mafuta ya MT.Ukombozi II ambayo iliwasili Nchini Agost 7 mwaka huu.

Alisema Meli hiyo mpya ya mafuta ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais Dk Shein imegharimu kiasi cha Euro 14,324,000 ambayo inauwezo wa kubeba tani 35,000 za mafuta.

“Meli hiyo imetengenezwa na kampuni ya DAMEN SHIPYARD ya nchini uholanzi Nchini China ambapo meli yetu hiyo inaurefu wa mita 86.2” alisema Mustapha Aboud Jumbe.

Mustapha Aboud Jumbe alisema kuwa kuwasili kwa meli hiyo inakamilisha ahadi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa Ilani Chama Cha Mapinduzi CCM 2015-2020.

“Katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015/2020 iliyozungumzia kuliimarisha shirika la meli ili iliweze kujiendesha kibiashara nkununua meli mpya Moja ya abiria na moja ya mafuta” alieleza Mustapha Aboud Jumbe.

Alieleza kuwa Meli ya Abiria ya Mv Mapinduzi tayari imeshanunuliwa na Serikali tangu mwaka 2015.

Aidha katibu Mkuu huyo alibainisha kuwa mazungumzo ya utengenezaji wa meli hiyo yalianza mnamo mwaka 2016 na matengenezo yalianza mwaka 2018 na kumilika mwaka huu 2019.

Katika Sherehe za Uzinduzi wa meli hiyo mpya ya Mafuta Rais Atapata fursa ya kuikagua na  kukata utepe kuashiriashiria Uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages