Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
KONGAMANO
la tatu la sekta ya mafuta na gesi litakalofanyika Oktoba 2 na 3 katika
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijiji Dar es Salaam
litazikutanisha nchi 67 ambazo zitawaweka pamoja wadau na viongozi
muhimu wa sekta ya nishati kutoka serikalini na sekta binafsi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Afisa mtendaji mkuu wa
Kampuni ya Ocean Business Partners na mwenyekiti wa jumuiya ya watoa
huduma ya nishati ya mafuta na gesi nchini Balozi Abdulsamad Abdulrahim
amesema kuwa malengo ya kongamano hilo ni pamoja na kuunga mkono
jitihada za Rais Dkt. John Joseph Magufuli ambaye daima amekuwa
akihamasisha kujenga nchi ya viwanda na kuipeleka nchi kwenye uchumi wa
kati.
"Tutaendelea
kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais na kupitia kongamano hili
tunategemea kufukua ajira, bunifu mbalimbali pamoja kuweka mahusiano
bora ya kibiashara baina ya wazawa na wageni" ameeleza Abdulsamad.
Amesema
kuwa kongamano hilo litakalowakutanisha washiriki zaidi ya 600
litachambua umuhimu wa kimkakati na nafasi ya Tanzania kama kitovu cha
Afrika Mashariki katika uendelezaji mkubwa wa sekta ya nishati.
"Washiriki
wa kongamano hili watapata fursa ya kufahamu hali ya sasa ya sekta ya
nishati nchini, mikakati ya kufikia Tanzania ya viwanda pamoja na
kujifunza namna ya kufanya makubaliano ya kibiashara baina ya makampuni
ya kimataifa na yale yaliyoko nje ya nchi" ameeleza Abdulsamad.
Amesema
kuwa mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo mipango ya muda mfupi ya
usambazaji na uhitaji wa nishati nchini, ushiriki wa wajasiriamali
wadogo katika sekta hiyo pamoja na ushirikiano baina ya serikali na
sekta binafsi katika kuyafikia malengo na hiyo itaenda sambamba na
utoaji wa tuzo maalumu kwa baadhi ya washiriki.
"
Tuzo mbalimbali zitatolewa ikiwemo tuzo kwa kampuni bora nchini,
kampuni bora ya kimataifa na kampuni bora ya mfano ya wazawa pamoja na
tuzo nyingine kwa wanafunzi wa vyuo walioshinda katika mashindano ya
insha ambao watapata ufadhili wa masomo ili kuendeleza vyema sekta hii
na pia mwanamke shupavu katika sekta hiyo na tutawasajili wanawake wote
ili kutoa chachu kwa wanawake wengine" ameeleza.
Balozi
Abdulsamad amesema kuwa viongozi mbalimbali wa wa Serikali wakiongozwa
na waziri wa nishati Dkt. medard Kalemani watashiriki katika kongamano
hilo ambalo pia limetoa fursa za kutangaza vivutio vya utalii na kutoa
ajira na fursa mbalimbali za kiuchumi kwa watanzania.
Mwenyekiti
wa jumuiya ya watoa huduma ya nishati ya mafuta na gesi nchini na Afisa
mtendaji mkuu wa Kampuni ya Ocean Business Partners Balozi
Abdulsamad Abdulrahim na Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na
kongamano la tatu la sekta ya mafuta na gesi na kueleza kuwa fursa
zaidi ajira na uwekezaji zinategemewa kupatikana kupitia kongamano hilo,
leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇