UONGOZI wa Benki ya NMB umesema kuwa
unazidi kuboresha mifumo ya huduma zao za kadi ili kuhamasisha watalii
pamoja wananchi wa kawaida kutumia kadi kwenye malipo na ununuzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya
Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir wakati akizungumza
kwenye maonesho ya Utalii visiwani Zanzibar, ambapo benki hiyo ni moja
wapo ya mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyofika
tamati siku ya Jumamosi.
Alisema kutokana na ukuaji wa Teknologia
Duniani, ndivyo wanavyo buni mbinu zitakazo wawezesha wateja wao kupata
huduma bora na za kimataifa. Vilevile,
mifumo ya Kidigitali na matumizi ya kadi
za MasterCard ambazo zinatumika kitaifa na kimataifa zimekua zikiondoa
usumbufu kwani huduma hizo zinaweza kutumikaa ndani na nje ya nchi.
Benki ya NMB benki hivi sasa ipo karibu
na wananchi mjini na vijijiNI hivyo kuingia katika masauala ya utalii,
kwa kiasi kikubwa itasaidia kuzidi kujitangaza na kuvutia wateja wengi
zaidi pamoja na wageni wanaofika nchini.
Naye Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar-
Balozi Seif Ali Iddi ameomba mashirikiano na taasisi nyingine katika
kutangaza utalii wa Zanzibar ili kuongeza idadi kubwa ya watalii
Zanzibar.
Alisema wananchi wa Zanzibar wananufaika
na utalii kupitia sera ya Utalii kwa wote na kubainisha kuwa sera hiyo
ipo wazi kuweza kunufanisha wananchi hasa kwa kuwa na usalama wa nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utalii
na Mambo ya Kale- Mahamoud Thabiti Kombo alisema kuwa maonyesho hayo ni
agizo la Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, ambapo lengo ni
kuitanganza Zanzibar kiutalii baada ya mafanikio
makubwa ya waka jana.
Alisema kuwa maonesho ya kila mwaka
yanawasadia wajasiriamali wadogo wadogo kujitangza kupitia utalii ili
waweze kunufanika na matunda ya utalii kwa kuuza bidhaa na kukuza
biashara zao.
Kwa upande wake Meneja wa NMB tawi la
Zanzibar - Abdalla Duchi, amewataka wananchi wa Zanzibar kuchangamkia
fursa za utalii zinazopatika nchini ili kujikwamua na umaskini .
Amewataka wajasiriamali wadogo wadogo na
wa kati kutumia fursa zinazotolewa na Benki hiyo katika maeneo
mbalimbali kwa kujisajili kuwa mawakala, ambapo itafungua fursa za ajira
sambamba na kutoa huduma kwa wananchi wa kawaida
ikiwemo watalii wanaokuja kutembea Zanzibar.
Aliongeza kuwa benki ya NMB ina wateja zaidi ya milioni tatu huku ikiongoza kwa matawi mengi -
229 nchini, yakiwemo NMB Zanzibar, NMB Mwanakwerekwe na NMB Chakechake- Pemba, huku ikiwa na jumla ya mawakala
84 Zanzibar kwa jumla ya idadi ya mawakala 6000 nchi nzima.
Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mheshimiwa Mahmoud
Thabit Kombo akizungumza na Maofisa wa Benki ya NMB alipotembelea banda
la benki hiyo kwenye Maonesho ya pili ya 'Zanzibar Tourism Show'
Visiwani Zanzibar.
Maofisa wa Benki ya NMB wakifurahi pamoja na Waziri wa Habari, Utalii,
Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo baada ya
kukabidhiwa cheti cha shukrani kwa udhamini wao.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (mwenye miwani)
akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd
wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya pili ya 'Zanzibar Tourism Show'
Visiwania Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇