Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kulia akimueleza jambo Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba wakati wa ziara yake wialayani humo |
MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange |
NAIBU
Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisalimiana na Naibu Waziri wa
Maji na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Pangani Seif
NAIBU
Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisialimiana na Katibu Tawala wa
wilaya ya Pangani Mwalim Hassani Nyange wakati wa ziara yake ya siku
moja wilayani humo
NAIBU
Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisalimiana na Afisa Tawala wa
wilaya ya Pangani Gibson George wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisalimiana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi
NAIBU
Waziri wa Kilimo Omari Mgumba amewataka walimu wa shule za Msingi na
Sekondari waache kutumia kilimo kama adhabu ya kuwapa wanafunzi wakati
wanapokosea kwani inawajengea tafsiri mbaya kwa jamii na baadae
wanapokuwa wanachukia kilimo.
Mgumba
alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake wilayani Pangani
ambapo alisema kwamba kuna tabia ambayo imejengeka kwa walimu hao kwamba
mtoto anapokosea anaambiwa leo utakwenda kilima siku nzima, utakwenda
kumwagilia hali ambayo inapelekea baadae wakikua wanakuwa hawahitaji
kilimo kwa sababu awali waliona kama adhabu.
Alisema
kwamba hapana suala hilo sio jema na ndio maana wao wanasema kilimo ni
ute wa mgongo lakini watafungamanisha kilimo na elimu ili watoto tokea
anakuwa ajue kwamba nchi hii uchumi wake unategemea kilimo.
“Hivyo
ninapoambiwa niwe na tuta la mchicha sio adhabu bali ni sehemu ya
kuniandaa kielimu nije kujitegemea au nije kuajiri wengine kwenye
mashamba yao kwani bila kufanya hivyo tutakuwa tunaimba kitu kingine
wakati uchumi wetu unategemea kilimo”Alisema Naibu Waziri huyo.
Naibu
Waziri huyo alisema kwamba mkakati wa serikali ni kuimarisha kilimo
hivyo wataendelea kufungamanisha elimu yao na kilimo chao.
Akizungumzia
Kilimo cha Minazi wilayani humo Naibu Waziri huyo alisema kwamba kilimo
cha minazi ni kweli mpaka sasa hawaapata ufumbuzi wa magonjwa yake kwa
miaka zaidi ya 30 mpaka leo ambayo yanasababsihwa na mabadiliko ya tabia
ya nchi.
Alisema
pia hilo linatokana na kukubali kuletewe mbegu ya kisasa ambayo
haiendani na mazingira ya nchi hivyo kama Taifa wameendelea kuimarisha
vituo vyao vya utafiti hasa cha utafiti wa minazi mikocheni lengo ni
kuanza kurudi kwenye kuzalisha miche kutumia minazi ya asili
inayokabiliana na hali ya hewa na ikolojia ya ya nchi yetu .
“Na
sasa tumeanza kuzalisha kitalu cha miche asili Bagamoyo na itasambazwa
nchi nzima kwa lengo la kupanda na hatimaye kuweza kurejesha minazi
hiyo”Alisema
Akizungumzia
udogo wa bei ya nazi nchini Naibu Waziri huyo alisema kwamba nazi
zinauzwa bei ndogo na imeendelea kuwa ndogo ni kutokana na ushindani
uliopo kwenye soko la ndani, kanda na kimataifa kwa sababu ya bidhaa
mbadala.
“Hivyo
kila nazi ikipanda bei watu wanakwenda kutumia mafuta lakini kila
tunapoacha kutumia nazi na kutumia mafuta na kwenda kwenye chukuchuku
wanapunguza mahitaji ya nazi”Alisema.
Hata
hivyo alisema kwamba wanakuja na mkakati wa kuanzisha viwanda ambavyo
vitaongeza thamani bidhaa hiyo ili kupanua soko la nazi hapa nchini na
mbegu za nazi ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi
huku akieleza kwamba wakienda kuongeza thamai tatizo hilo litakwisha.
Katika
hatua nyengine Naibu Waziri huyo aliwataka watanzania tuendelee kutumia
nazi kwani wanapoendelea kuitumia zaidi wanatongeza mahitaji na soko la
nazi litakuwa kubwa huku akisistiza kwamba watakaendelea kutumia mafuta
bei ya nazi itashuka.
Awali
akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa
Aweso alisema kwambazao la nazi limeathiriwa namaradhi kwa muda mrefu
mpaka yamepatikana bado tiba yake haijapatikana miaka 30.
Alimwambia
Naibu Waziri Mgumba kwamba ugonjwa huo umekuwa haupati ufumbuzi kama
lilivyokuwa gonjwa la ukimwi hiyo walimuomba watafiti na watalamu
wafanye utafiti ambao utafika mwisho na wenye manufaa na kuweza
kurudisha uchumi wake.
“Kwa
sababu nazi zinakazi nyingi unaweza kusingwa na machicha yake ukabaki
hapa Pangani….lakini pia inaleta heshima kwenye ndoa na hivyo kuweza
kurejesha furaha”Alisema.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇