Sudan ilisimamishwa uanachama wake katika Umoja wa Afrika mwezi Juni kufuatia vurugu za maandamano ambapo madaktari wa upande wa upinzani walisema watu kadhaa waliuwawa katika vurugu hizo kati ya jeshi na upinzani.
Lakini baada ya jeshi na vyama vya kiraia pamoja na viongozi wa maandamano kutia saini mkataba wa miaka mitatu, wa kugawana madaraka mwezi Agosti, Sudan ilimteua Abdalla Hamdok kuwa Waziri Mkuu.
Siku ya Alhamisi Hamdok aliunda baraza la kwanza la mawaziri nchini humo tangu mwezi Aprili wakati Omar al Bashir alipoondolewa madarakani.
Katika Mkutano uliofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika lilipiga kura kuiondoa Sudan katika kikwazo hicho ilichowekewa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇