LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 7, 2019

POLISI WASAMBAZWA KUZUWIA MAANDAMANO KATIKA UWANJ WA NDEGE

Polisi wa kukabiliana na ghasia wamesambazwa mjini Hong Kong leo Jumamosi ili kuzima mipango ya waandamanji wanaodai demokraia waliolenga uwanja wa ndege katika hatua ya kwanza ya vuguvugu hilo kuushawishi umati mkubwa wa wandamanaji tangu kiongozi wa eneo hilo alipotangaza muafaka wa ghafla mapema wiki hii.

Mamilioni ya watu wameandamana mjini Hong Kong kwa miezi mitatu sasa na kusababisha changamoto kubwa kwa utawala wa China tangu ulipokabidhiwa eneo hilo kutoka kwa Uingereza mwaka 1997.

Siku ya Jumatano kiongozi wa HongKong Carrie Lam aliwashangaza wengi aliposema anaifuta sheria tata iliyohusu kuwapeleka watuhumiwa kushtakiwa China Bara, hatua iliyoanzisha maandamano makubwa na ambayo wakati mwingine yanageuka kuwa ya vurugu.

Polisi waliimarisha usalama katika maeneo ya kuabiri mabasi, feri na treni wengi wakiwa wamevalia mavazi ya kukabiliana na ghasia na kupekuwa mikoba ya vijana na kuhakiki vitambulisho vyao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages