Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera imefanikiwa kwa asilimia 98 kukamilisha maandalizi ya Mitihani kwa wahitimu wa darasa la saba 2019 unaotarajiwa kufanyika Septemba 11-12 Mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 7, 2019, na Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Mhe. Hashim Murshid Ngeze waka akiongea na vyombo vya habari katika Ofisi za halmashauri hiyo zilizopo mkoani hapa
Ngeze amesema hadi sasa Mitihani hiyo tayari imeishawasili wilayani humo na zoezi la kuingawa kwenda shule za msingi ili kila shule iweze kuipata mitihani yake ambapo pia kiasi cha fedha kwa ajili ya kusimamia mitihani hiyo tayari zimeletwa na bajeti imeishakuwa tayari maandalizi yako vizuri na kutaja maandalizi hayo kwakia asilimia 98.
Mhe. Ngeze amesema Halmashauri hiyo ina shule 141 za kiserikali na 8 za binafsi huku akitaja jumla ya wanafunzi ambao wanatarajia kufanya mitihani wilayani humo kuwa wasichana ni 3511 na wavulana ni 3351.amesema
Anatarajia matokeo mazuri sana kwa hivi karibuni serikali imetoa pikipiki kwa waratibu wa elimu kata kwa hiyo ufuatiliaji wa shule ya msingi unaenda vizuri ambapo amedai kuwa hata kwa mitihani ya ndani wa shule ya msingi kujipima
Wanafunzi walifanya vizuri kutokana na usimamizi mzuri.‘’Wito wangu kwa wazazi na walezi wa watoto wanaotarajia kufanya Mitihani huoni kuwa karibu na watoto kuwaliwaza, ili wasiwe na mawazo wakiwa ndani ya chumba cha Mtihani kwa sababu kushindwa kwa mtihani kunaanzia na maandalizi ya mtoto kutoka nyumbani
Anapoingia ndani ya chumba cha Mtihani ana mawazo jambo hilo linalosababisha kushindwa kufuata maelekezo ya mtihani , kwa hiyo wazazi kwa kipindi hiki toeni uhuru kwa watoto wenu na mkawape ushauri wa jinsi ya kutulia na kufanya mitihani yao vizuri,,’’amesema
Amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wazazi wanaowashinikiza watoto wao wasifanye vizuri mitihani yao ili kushinda kuingia kidato cha kwanza
kwa sababu ya umbali mrefu wa kufuata shule huku akitolea mfano shule ya msingi Kasharu na Rukoma kuwa hilo limekuwa likifanyika.
Ameongeza kuwa alitembele shule ya msingi Kamukore kati ya wanafunzi 19 wanafunzi 7 walikiri kwamba wazazi wao wameishawaambia wasifanye vizuri mtihani wao wa darasa la saba kwa sababu ya ukosefu wa shule ya sekondari amewataka wazazi kutolipa kipaumbele suala hilo
Ili watoto wao wapate elimu sitahiki na kutimiza ndoto zao.Amesema zaidi ya shilingi milioni 600 zimepokelewa kutoka serikali ili kuwezeshaelimu bila malipo na kumshukuru Rais wa jamhuli ya muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli kwa kuanzisha utaratibu wa elimu bila malipo kwa sababu inaondolea wazazi mzigo wa kulalamika.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇