LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 8, 2019

SHAMBULIO DHIDI YA GAZA, JINAI INAYOKARIRIWA NA ISRAEL

Katika miezi ya hivi karibuni, utawala huo ghasibu umekuwa ukiendesha vita vya jinai dhidi ya makundi ya mapambano ya Kiislamu katika eneo la Asia Magharibi. Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo wa kibaguzi na ambaye mwezi Mei uliopita alishindwa kubuni serikali mpya amebadilisha vita vya jinai kuwa chombo chake cha kuendeshea kampeni za uchugzu ambao umepangwa kufanyika tarehe 17 mwezi huu. Kupitia vita hivyo, Nertanyahu anajaribu kuwathibitishia walowezi wa Kizayuni wanaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina kwamba ni yeye tu ndiye anayeweza kudhamini usalama wa Israel na kukabiliana na makundi ya mapambano ya Kiislamu katika eneo. Pamoja na hayo lakini shambulio lililofanywa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon tarehe Mosi mwezi huu dhidi ya wanajeshi wake katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel) lilivunja na kupunguza makali ya propaganda hizo za Netanyahu.
Licha ya hayo, mtawala huyo wa Kizayuni angali anasisitiza kutumia mbinu hiyo ya vita na hivyo kuamua kuendelea luushambulia Ukanda wa Ghaza ili kufikia malengo yake ya uchaguzi. Amri ya kufanyika shambulio hilo imetolewa na Netanyahu ambaye pia kwa sasa anasimamia Wizara ya Vita ya utawala wa Kizayuni, katika hali ambayo mwezi Mei uliopita alilazimika kukubali usitishaji vita katika ukanda huo baada ya kupita siku mbili tu za vita.
Mji wa Ghaza ukishambuliwa na Wazayuni
Msemaji wa jeshi la Israel amedai kuwa mashambulio ya leo alfahiri yamefanyika katika kujibu upenyaji wa  ndege moja isiyo na rubani ya Hamas katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo na kulishambulia gari moja la kijeshi, suala ambalo limekanushwa na makundi ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina yakisema kuwa lengo la uchokozi huo wa Israel ni kufanikisha kampeni za uchaguzi za Netanyahu. Jambo hilo pia limethibitishwa na wanasiasa wa Israel ambao wamekuwa wakimkosoa sana Netanyahu kwa kuanzisha pia uchokozi dhidi ya Hizbullah ya Lebanon.
Kuhusiana na suala hilo, Yair Lapid, mwanasiasa mashuhuri wa Israel amemkosoa vikali Benjamini Netanyahu kuhusiana na hali ya usalama ya hivi sasa ya utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa hali hiyo inatokana na siasa zake mbovu na za kipropaganda. Amesema: Mabalaa yanayotuteremkea leo na kuwafanya watu wakimbilie mapango ya salama ni siasa zilizojaa makosa za Netanyahu. Lapid amemtuhumu Netanyahu kwamba amekuwa akitekeleza siasa za hadaa na kukataa kuwajibika kuhusiana na hatua zake za kijeshi ili kufikia malengo ya kisiasa. Amesema ili kufikia melengo hayo na kuvutia kura za raia katika uchaguzi ujao, Netanyahu amekuwa akihatarisha moja kwa moja maisha ya wanajeshi wa Israel kwa kuwasukuma kwenye moto wa kukabiliana na Hizbullah.
Makombora ya Hamas
Inaonekana kuwa Netanyahu ameamua kufuata njia ya kijeshi na kuyachokoza makundi ya mapambano ya Kiislamu kutokana na ukweli kwamba hawezi kuendesha kampeni za uchaguzi za kawaida kwa kuwa anakabiliwa na kashfa nne muhimu za ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma. Wapinzani wake wa kisiasa wanatumia kashafa hizo kumpiga vita, jambo ambalo limemlazimisha kuchukua njia ya kijeshi kukabiliana nao katika uwanja wa kuwania kura za Wazayuni.
Pamoja na hali hiyo, ni wazi kuwa Netanyahu anapasa kusubiri jibu la makundi ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina. Ulyur Livi mchambuzi wa tovuti ya habari ya gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronot anasema kuhusiana na suala hilo: Hamas inatambua vyema mashambulio yanayofanywa na ndege za kivita za Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza, kinyume na kanuni na uwiano wa kivita kati ya kundi hilo na Israel, hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa itafanya mashambulio ya kulipiza kisasi kutokea ukanda huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages