LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 8, 2019

RAIS WA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN AIPONGEZA JAMHURI YA WATU WA CUBA

Jamhuri ya Watu wa Cuba imepongezwa kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya na kuelezwa haja ya kutoa nafasi za masomo ya Udaktari Bingwa kwa Madaktari wa Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo wakati alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Kwanza wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Watu wa Cuba Marcelino Medina Gonzalez, Ikulu mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Shein alizipongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Cuba katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo ikiwa ni pamoja na kuiunga mkono Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo sekta ya afya.

Hivyo, Rais Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa Zanzibar inathamini sana mashirikino hayo yaliopo hasa katika sekta ya afya ambapo nchi hiyo imo katika mashirikiano na Zanzibar ya kusomesha Madaktari ambapo tayari kuna Madaktari 15 wa Zanzibar wanasoma nchini humo hivi sasa katika Chuo Kikuu cha Mantanzas.

Kutokana na juhudi hizo, Rais Dk. Shein alieleza haja ya kuendelezwa mashirikiano zaidi kwa Jamhuri ya Watu wa Cuba kutoa nafasi ya masomo ya Udaktari Bingwa kwa Madaktari wa Zanzibar hasa ikizingatiwa kuwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimeshaanza kutoa wahitimu mabali mbali wa fani hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages