LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 1, 2019

MAWAZIRI WA RWANDA NA UGANDA KUKUTANA ILI KUJADILI MAKUBALIANO YA LUANDA, ANGOLA

Imeelezwa kuwa, lengo la mkutano huo ni kuangalia namna ya kuyafanyia kazi makubaliano ya kumaliza uhasama yaliyotiwa saini hivi karibuni baina ya Rais Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda.
Duru za karibu na nchi hizo zinasema kuwa, mkutano wa kwanza wa ngazi za juu baina ya pande mbili unatarajiwa kufanyika katika kipindi cha majuma machache yajayo.
Pande zote mbili zina uhakika kwamba, makubaliano hayo ya Luanda, Angola yatatekelezwa, zimeeleza duru hizo.
Agosti 21 mwezi uliopita, Marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda walisaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda yenye lengo la kumaliza uhasama na mzozo uliopo kati ya mataifa hayo mawili jirani.
Marais wa Rwanda na Uganda ambao hivi karibuni walitiliana saini makubaliano ya kumaliza uhasama
Marais hao walifikia makubaliano hayo katika mkutano wa pili huko Luanda mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Angola na Congo Brazaville waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.
Joto la mzozo baina ya Rwanda na Uganda limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na limeathiri maisha ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.
Maafisa nchini Rwanda wamekuwa wakiituhumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaituhumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages