Televisheni ya al Manar imetangaza kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeangamiza moja ya zana za kijeshi za Israel katika barabara ya al Thakna katika mji wa mpakani wa Israel wa Avivim na kumuua kamanda wa kikosi kimoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni huko kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu katika oparesheni iliyotekelezwa na harakati ya Hizbullah.
Hizbullah imetoa taarifa ikieleza kuwa kundi la mashahidi Hassan Zebib na Yassir Tahir ndilo lililotekeleza oparesheni hiyo. Televisheni ya al Aalam pia imeripoti kuwa jeshi la Israel limewaagiza wakazi wa maeneo ya mpakani na Lebanon kusalia majumbani. Televisheni ya al Jazeera pia imevinukuu vyombo vya habari vya jeshi la Israel na kutangaza kuwa: Jeshi hilo limewataka wakazi wa maeneo ya kandokando na mipaka ya Lebanon yaliyoko katika umbali wa kilomita nne.
Ripoti zilizotufikia zinasema kuwa, Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Israel ameelekea katika Wizara ya Vita ya utawala huo kwa ajili ya kikao cha dharura pamoja na wakuu wa majeshi na wa idara za intelijinsia za utawala ili kufuatilia hali ya mambo inayoendelea sasa katika mipaka ya Lebanon.
Vyombo vya habari vya Lebanon aidha vimetangaza kuwa jeshi la Israel limetumia risasi zenye mada za fosiforasi kushambulia maeneo ya kandokando mwa Maroun al Ras kusini mwa Lebanon.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇