Vitendo vya mauaji katika matukio ya ufyatuaji risasi nchini Marekani vinazidi kuongezeka kila siku ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja pekee watu wasiopungua 51 wameuawa nchini humo.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, watu 51 wameuawa nchini Marekani katikka kipindi cha mwezi mmoja pekee kufuatilia matukio mbalimbali ya ufyatuaji risasi nchini humo.
Gazeti la New York Times la nchini Marekani limeashiria katika ripoti yake kuhusiana na ufyatuaji risasi mkubwa nchini humo na kueleza kwamba, mwezi uliopita wa Agosti ulishuhudia mauaji makubwa ambapo watu 51 waliuawa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kufuatia matukio ya ufyatuaji risasi.
Matukio ya ufyatuaji risasi nchini Marekani hutokea mara kwa mara katika miji na majimbo tofauti ya nchi hiyo na kupelekea maafa makubwa.
Maelfu ya raia wa Marekani huuawa kila mwaka katika matukio ya mashambulizi ya silaha za moto katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Vitendo vya ukatili wa silaha za moto nchini Marekani vimegeuka kuwa moja ya matatizo makubwa na sugu katika jamii ya Marekani ambayo imezoea kuzinyoshea kidole cha lawama nchi nyingine za dunia kuhusiana na ukosefu wa amani.
Ushawishi wa lobi zenye nguvu za utengenezaji silaha katika serikali na kongresi ya Marekani umevuruga juhudi zote zinazofanywa na makundi ya kutetea haki za binadamu zinazolenga kubuniwa sheria kali za kudhibiti umiliki wa silaha nchini humo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇