Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 27 Septemba 2019.
(Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Songwe Serikali imesema kuwa inaimarisha mikakati yake ili kuwa na uwezekano wa kuwa na malighafi toshelevu katika viwanda vyote nchini.
(Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Songwe Serikali imesema kuwa inaimarisha mikakati yake ili kuwa na uwezekano wa kuwa na malighafi toshelevu katika viwanda vyote nchini.
Ifahamike
kuwa malighafi nyingi zinazotumika viwandani asilimia kubwa zinatokana
na sekta ya kilimo hivyo moja ya mkakati madhubuti ni kusimamia kwa
weledi sekta hiyo ili kuwa na malighafi nyingi na za kutosha. Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 27 Septemba
2019 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
eneo la Vwawa Mkoani Songwe.
Alisema
kuwa miongoni mwa majukumu muhimu ya Wizara ya kilimo ni kuimarisha
Mchango wa sekta ya kilimo ili wakulima waweze kuongeza uzalishaji na
tija. "Ni lazima tuhakikishe kuwa watu wanazalisha kwa ajili ya biashara
sio chakula pekee na gharama wanazotumia ni lazima wahakikishe zinarudi
ili waone faida ya kilimo" Alikaririwa Mhe Hasunga Waziri Hasunga
ameeleza kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo ina jukumu la
kuhakikisha umasikini unapungua kwa kuongeza uzalishaji kwa wakulima ili
kilimo kiendelee kuingiza fedha nyingi za kigeni na kuchangia kwa wingi
pato la Taifa.
Kadhalika
ametaja Mikakati mingine ya wizara ya kilimo kuwa ni pamoja na Pembejeo
(Mbegu bora, Mbolea, na Viuatilifu) kufika kwa wakati kwa wakulima
ambapo amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kununua mbegu Bora kwani
zinaweza kukinzana na magonjwa na nyingi zinastahimili ukame. Kuhusu
masoko ya mazao ya wakulima waziri Hasunga amesema kuwa wizara yake
imekuja na mkakati maalumu wa kuanzisha kitengo cha masoko kitakachokuwa
na majukumu ya kubainisha masoko ya mazao mbalimbali ya wakulima.
"Ni
lazima kufanya biashara kisasa kwa kujua mahitaji ya soko kabla ya
kuzalisha mazao ya kilimo ili wakulima wanapozalisha tayari wawe wanajua
watauza wapi mazao yao" Alisisitiza Mhe Hasunga Katika mkutano huo
uliohudhuriwa na mamia ya wananchi ambao ni wakazi wa mamlaka ya mji
mdogo wa Vwawa na ameneo ya jirani, Waziri Hasunga amewataka wananchi
kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa
na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kuimarisha ufanisi wa
shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa na Taifa kwa ujumla.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 27 Septemba 2019.
(Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇