Mratibu
wa Kongamano la kuombea nchi amani kutoka Taasisi ya Mudir Markaz
Safina, Sheikh Said Kinyogoli (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu Kongamano hilo mjini hapa jana.Kulia ni Sheikh Najim
Humoud na kushoto ni Imamu Sheikh Abubakar Masuala. (Picha Boniphace
Jilili).
Na Boniphace Jilili, Singida
Kongamano kubwa la kuiombea nchi amani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika mkoani Singida.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa, Mratibu wa Kongamano hilo Sheikh
Said Kinyogoli alisema limeandaliwa na TaasAsi ya Mudir Markaz Safina
chini ya baraza kuu la waislam Tanzania (Bakwata),lengo likiwa ni
kuiombea nchi amani katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
"Panapo
kusekana amani hauwezi kufanya jambo lolote liwe la kijamii na la
kimaendeleo kwani ukijaribu mara unasikia bomu linalipuka kwasababu
hakuna amani." alisema Sheikh Kinyogoli.
Sheikh
Kinyogoli alisema kongamano hilo litafanyika kwa siku saba katika
viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi mjini hapa, kuanzia siku ya
jumatano wiki hii na litashirikisha watu wote bila kujali itikadi za
kidini, ambapo watakuwepo masheikh, Hilary Kipozeo, Hashim Mbonde na
Mzee Yusuph wote kutoka Dar es salaam.
Wengine
ni Sheikh Jafari Abdulahaman kutoka Morogoro, Sheikh Mohamed
Makarani-Mwanza pamoja na Sheikh Ibrahim Mlumbango kutoka Kigoma.
Alisema
sanjari na kuiombea nchi amani pia watakuwa wanaadhimisha mwaka mpya wa
kiislam ambapo watatoa nasaha za kidini ili watu wawe na hofu ya Mungu.
Sheikh
Juma aliongeza kuwa katika kongamano hilo yatatolewa mafunzo ya
ujasiriamali kwa ajili ya watu kujifunza mbinu za kujitegemea kwa
kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji ili kujiinua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇