Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji
Mhe.Angellah Kairuki akioneshwa namna mfumo wa TEHEMA unavyorahisisha
utendaji kiwandani hapo na Mhandisi Brezil Omary wakati wa ziara yake
kiwandani hapo.
Sehemu
ya wajumbe waliposhiriki katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki wakati wa
ziara yake katika kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Sekta ya Uzalishaji Balozi Celestine Mushi akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
Viwango
wa Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote Bw. Issawema akiwaonesha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji
Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula matumizi ya mifumo ya TEHAMA
katika kuendesha kiwanda hicho.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji
Mhe.Angellah Kairuki akisisistiza jambo kwa uongozi wa kiwanda cha
kutengeneza Saruji cha Dangote kilichopo Mkoa Mtwara alipotembela
kukagua na kusikiliza changamoto za wawekezaji mkoani humo.Katikati ni
Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw.Jagat Rathee.
…………………………………………………….
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe.
Angellah Kairuki ametoa muda wa wiki moja kwa Kiwanda cha kutengeneza
saruji cha Dangote kuwasilisha taarifa ya utendaji ambazo kwa zaidi ya
miaka miaka mitatu hawajaziwasilisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
kama sheria na taratibu za nchi zinavyoelekeza.
Waziri
Kairuki ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula Katika ziara yake ya
kutembelea, kukagua maeneo mbalimbali ya uwekezaji na kuongea na
wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Lindi septemba 27,2019
ameuelekeza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kila baada ya miezi
sita wanawasilisha taarifa za kiutendaji TIC.
Waziri
Kairuki aliwaeleza masikitiko yake viongozi wa kiwanda hicho kwa
kutowasilisha taarifa za utekelezaji wao ikiwemo zinazohusu historia ya
mradi, mipango ya upanuzi, kodi wanazolipa, faida pamoja na changamoto
wanazokabiliana nazo na ushauri wao.
“Nimesikitishwa
sana na suala hili la kutopeleka taarifa zenu TIC ambapo inafahamika
suala hilo ni la kisheria na lazima litekelezwe kwa wakati,hivyo kuanzia
sasa nimewapa wiki moja mhakikishe taarifa hizo zinawasilishwa
haraka,”alisisitiza Waziri Kairuki.
Aidha
amewapongeza Dangote kwa uwekezaji huo mkubwa pamoja na kuanza ujenzi wa
mradi wa kuzalisha umeme wao wenyewe megawati 25 ambao megawati 5
zitaingia kwenye gridi ya taifa.
Amewataka
wawekeze na maeneo mengine siyo kwenye saruji tu na kuagiza TIC kupitia
mikataba ya utendaji ya wawekezaji wote mahiri kuona ni wapi wanaweza
kuwekeza zaidi.
Wakiwa
Mkoani Lindi Waziri Kairuki na Mhe. Mabula walitembelea mgodi wa madini
ya uno (graphite) uliopo katika Kijiji cha Matambalale Kusini Wilaya ya
Ruangwamkoani Lindi na kuona shughuli za awali za mradi huo ambapo
Meneja wa kampuni ya Lindi Jumbo inayochimba madini hayo Bw Paul Shauri
amesema mgodi utajengwa kwa muda wa miezi tisa na wanatarajia kuwekeza
zaidi ya dola za kimarekani milioni 30.
Akiongea
mgodini hapo Dkt.Mabula ameziagiza Halmashairi zote vijiji vyenye
maeneo ya uwekezaji kufanya zoezi la kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi
watenge maeneo ya uwekezaji wayahaulishe yawe mali ya kijiji ili
mwekezaji akipatikana watimize masharti mengine tu.
“Hakuna
sababu ya mwekezaji kuanza kuhangaika na mambo madogo kama hayo ambayo
yanampotezea wakati ni lazima halmashauri zijipange ili kumwekea
mwekezaji mazingira mazuri avutiwe kuwekeza”alisema Dkt.Mabula
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa akiwakaribisha
Mawaziri hao amesema Serikali ione kuna sababu ya kuharakisha ujenzi wa
miundombinu ikiwemo barabara za wilaya hiyo kwani kuna makampuni mengi
makubwa yameonesha nia ya kuwekeza.
Amesema
wilaya hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya mipaka ya asili na kwamba
suala hilo tayari linaendelea kutatuliwa kwa viongozi na watendaji kutoa
elimu kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇