LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 28, 2019

WAHAJIRI 40 WAHOFIWA KUFARIKI DUNIA LIBYA BAADA YA BOTI YAO KUZAMA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi limesema tukio hilo la Jumanne limeifanya irejelee wito wake wa haraka wa kuchukua hatua za kuokoa maisha.
Manusura wapatao 60 wameokolewa na kupelekwa ufukweni katika mji wa pwani wa Al-Khoms, takribani kilomita 100 mashariki mwa Tripoli. Shughuli ya uokoaji iliyofanywa na walinzi wa pwani ya Libya pamoja na wavuvi imekuwa ikiendelea tangu asubuhi ya leo na bado inaendelea.
Vincent Cochetel, mwakilishi maalumu wa UNHCR katika eneo la Mediterania ya kati  amesikitishwa na maafa hayo na ametaka hatua zichukuliwe kuyazuia katika siku za usoni.
Timu za UNHCR zimenawapatia manusura msaada wa matibabu na wa kibinadamu. Tukio hili limekuja wiki chache baada ya tukio lingine la kuzama kwa meli ambapo maisha ya watu 150 yanakadiriwa kupotea katika tukio moja tu kwa mwaka huu katika bahari ya Mediterania.
Kufuatia janga la jana, inakadiriwa kuwa watu 900 tayari wamepoteza maisha wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania kwa mwaka huu wa 2019.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages