LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 28, 2019

MATESO KWA WANANCHI WA KASHMIR, INDIA YAPINGA UPATANISHI WA NCHI YOYOTE

Narendra Modi alisema hayo Jumatatu baada ya kuzungumza na rais wa Marekani, Donald Trump pambizoni mwa kikao cha G7 kilichofanyika nchini Ufaransa na kuongeza kuwa, masuala yote yaliyopo baina ya India na Pakistan yanazihusu nchi hizo mbili na hakuna haja kwa nchi yoyote ya tatu kuingilia masuala hayo.
Matamshi hayo ya Waziri Mkuu wa India ni majibu ya wazi kwa juhudi za Pakistan za kuiomba jamii ya kimataifa kuingilia kadhia
Jeshi la India linalaumiwa kwa kuwakandamiza wananchi wa Kashmir
ya Kashmir na kuruhusu pande mbalimbali kulitatua suala hilo. Katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, Islamabad imeongeza juhudi za kulifanya suala la Kashmir kuwa la kimataifa ikisisitizia ulazima wa kuruhusiwa upande wa tatu kutatua mgogoro huo wa miaka mingi. Juhudi hizo mpya za Pakistan zinafanyika baada ya serikali ya India ya Waziri Mkuu Narendra Modi kutangaza kuwa eneo la Kashmir linalodhibitiwa na nchi hiyo, litapokonywa utawala wa ndani, na kuwa sawa na maeneo mengine ya India. 
Pakistan imelaani vikali uamuzi huo wa upande mmoja wa India dhidi ya Kashmir na kutahadharisha kuhusu matokeo mabaya ya uamuzi huo ghalati. Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan amesema kuwa, uamuzi huo wa serikali ya India wa kulipokonya eneo la Jamu na Kashmir hali yake maalumu, ni kosa la kiistratijia na kama hali ya eneo hilo itaharibika, si India na Pakistan pekee zitakazodhurika, bali madhara yake yataenea dunia nzima. Licha ya Pakistan kutoa onyo hilo na kufanya juhudi za kuigeuza kadhia ya Kashmir kuwa ya kimataifa, lakini India hadi hivi sasa haijachukua hatua zozote za kupunguza hali ya wasiwasi katika eneo hilo na imeonesha kuwa haishughulishwi na maonyo hayo ya Pakistan. Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, India imepata uthubutu wa kuchukua hatua hiyo kutokana na uungaji mkono wa madola ya kigeni ya nje ya eneo hilo. Wachambuzi walio wengi wanasema kuwa, uamuzi wa New Delhi wa kulipokonya eneo la Jamu na Kashmir haki zake maalumu una uhusiano na uungaji mkono wa madola ya kigeni hasa Marekani kwa serikali ya Waziri Mkuu, Narendra Modi.
Jamu na Kashmir

Jarida la Foreign Policy la Marekani hivi karibuni lilikosoa vikali matamshi ya rais wa nchi hiyo, Donald Trump kuhusu kadhia ya Kashmir na kuandika:
Eneo lolote lililo na migogoro duniani, huukosi mguu wa Marekani ndani yake. Suala hilo limekuwa ni kigezo cha kudumu kwa Marekani, na kwamba matukio ya hivi sasa ya Kashmir nayo yana uhusiano na misimamo na vitendo vya rais wa Marekani.
Matamshi ya siku ya Jumatatu ya rais wa Marekani wakati alipoonana na Waziri Mkuu wa India huko Ufaransa, ni uthibitisho wa wazi wa uhakika huo uliosisitizwa na jarida la Foreign Policy la Marekani. Hivi karibuni Donald Trump alisema, yuko tayari kuzipatanisha India na Pakistan, lakini juzi Jumatatu alitia ulimi puani na kubadilisha msimamo wake wa awali akisema, India na Pakistan zinaweza zenyewe kutatua matatizo yao bila ya uingiliaji wa upande wa tatu. Ingawa msimamo huo mpya wa Donald Trump si wa kushangaza kwani hiyo ndiyo dhati ya rais huyo wa Marekani, lakini uhakika huu nao haupingiki kwamba siasa za Marekani kuhusu eneo la kusini mwa Asia, ni kuiunga mkono India kwanza kabla ya nchi nyingine yoyote. Yumkini ni kwa sababu hiyo ndio maana Waziri Mkuu wa Pakistan akaashiria katika matamshi yake ya juzi Jumatatu kwamba, madola makubwa duniani yana jukumu mbele ya kadhia ya Kashmir na ni wajibu wao kuwasaidia wananchi wanaodhulumiwa wa eneo hilo. Lakini kama madola hayo yatakataa kuwasaidia wananchi wa Kashmir, Pakistan itaendelea kuwa pamoja na wananchi hao madhlumu hadi pumzi ya mwisho.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages