LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 28, 2019

ZARIF: SIASA ZA MAREKANI DHIDI YA IRAN NA CHINA NI UGAIDI WA KIUCHUMI

Dk Mohammad Javad Zarif alisema hayo jana (Jumanne) mbele ya waandishi wa habari kabla ya kuondoka nchini China na kuongeza kuwa, Marekani haina nafasi yoyote katika eneo la Ghuba ya Uajemi na kwamba kuwepo kwake nchi hiyo katika eneo hilo ndiko kunakosababisha ukosefu wa amani na utulivu.
Aidha ameashiria mazungumzo yake na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na kusema kuwa, katika mazungumzo hayo pande mbili zimezungumzia uhusiano wao wa miaka 25 katika nyuga tofauti na nafasi ya Iran katika mradi wa "Mkanda Mmoja - Njia Moja."
Uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mzuri na wa kupigiwa mfano

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amegusia pia nafasi muhimu na ya kihistoria ya Iran katika njia maarufu ya hariri na kuongeza kuwa, maeneo ya "kusini - kaskazini," "kusini - magharibi" na "mashariki - magharibi" ya Iran yanaweza kutoa mchango mkubwa katika ustawi wa kieneo na wa dunia nzima.
Dk Zarif amezungumzia pia ziara yake ya siku mbili mjini Tokyo Japan na kusema kuwa ni ya kufuatilia maafikiano yaliyofikiwa katika ziara ya Abe Shinzo, Waziri Mkuu wa Japan mjini Tehran na kutoa nafasi kubwa zaidi kwa Japan ya kushiriki katika uchumi wa Iran na masuala mengine yanayohusiana na nchi hizi mbili.
Baada ya China, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameelekea nchni Japan kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa ustawi wa bara la Afrika. 
Mkutano huo wa siku mbili ulinza jana Jumanne katika mji wa Yokohama, wa kusini mwa mji mkuu wa Japan, Tokyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages