Mwanamume mmoja mkazi wa Tandale kwa Mtogole jijini Dar es Salaam, Siasa Samwel (30), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kumjeruhi kwa kumkata kwa viwembe sehemu za siri mwanamke mmoja ambaye jina linahifadhiwa
Novemba 15, 2018 mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkata mwanamke huyo sehemu za siri na kumsababishia maumivu. Mbele ya hakimu Boniface Lihamwike, wakili wa Serikali, Veronica Mtafya alidai.
Mtafya amedai upelelezi wa kesi hiyo unaendelea huku mshtakiwa huyo akikana kuhusika na tukio hilo.
Wakati hakimu Lihamwike akisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa, Samwel amesema hana mdhamini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake. Mshtakiwa huyo alirudishwa rumande na kesi hiyo kuahirishwa hadi Septemba 2, 2019.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇