Salamu za pongezi za kuchaguliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC zimeendelea kumiminika leo Agosti 20, 2019 ambapo Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) nayo imetoa salamu zake za pongezi.
CPB Yampongeza Rais Magufuli Kwa Kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti Mpya Wa SADC
"Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) tunatoa pongezi nyingi kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kwenye kikao cha 39 cha Wakuu wa Nchi za SADC jijini Dar es Salaam 2019.
Tunakutakia Mheshimiwa Rais kazi njema na yenye ufanisi katika kutekeelza majukumu hayo mapya." Taarifa hiyo imesema.
Katika kikao cha kihistoria cha siku mbili kilichofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 17 na 18, 2019, Wakuu hao wa Nchi walimchagua Dkt. Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipoindi cha mwaka mmoja ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa SADC Mhe. Dkt. Hage Gengob, ambaye ni Rais wa Namibia alimkabidhi uenyekiti huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇