Watu wawili wamefariki na wengine 50 bado wamekwama chini ya vifusi baada ya jengo lenye ghorofa nne kuporomoka mjini Mumbai nchini India hii leo.
Polisi wamesema watu watatu ikiwemo watoto wawili waliokolewa kutoka kwenye jengo hilo na wanaendelea kupokea matibabu hospitalini.
Jumla ya familia 10 hadi 12 walikuwa wakiishi katika jengo hilo lililojengwa miaka 80 iliyopita, kulingana na taarifa zilizotolewa na wakazi wa eneo hilo. Kuna uwezekano wa idadi ya vifo kuongezeka lakini shughuli za uokoaji bado zinaendelea.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇