LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 6, 2019

WATU ELFU MOJA WAUAWA LIBYA

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limetoa ripoti maalumu kuhusu suala hilo na kubainisha kuwa, tangu jenerali muasi Khalifa Haftar alipoanzisha mashambulizi dhidi ya mji kuu wa Libya Tripoli, mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu hadi hivi sasa, karibu watu 1000 wameshauawa kwenye mapigano.
Ripoti ya shirika hilo imeongeza kuwa, idadi ya wahanga wa mashambulizi ya hivi karibuni ya dhidi ya kituo cha kuhifadhia wahajiri mashariki mwa Libya imeshafikia 53. 
Ndege za kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar, mapema Jumatano asubuhi lilishabulia kituo hicho cha mjini Tripoli, cha kuhifadhia wahajiri waliongia Libya kinyume cha shria.
Mauaji ya kutisha yanaendelea nchini Libya tangu jenerali muasi Khalifa Haftar alipotangaza vita dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli tarehe 4 Aprili 2019. Watu 1000 wameshauawa hadi hivi sasa

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amezishutumu Imarati na Misri kwa kuhusika katika shambulizi dhidi ya kituo hicho cha kuhifadhia wahajiri wa kigeni.
Fathi Bashagha alisema jana (Ijumaa) katika mahojiano na gazeti la Marekani la Wall Street Journal kwamba bomu lililotumika kushambulia kituo hicho cha wakimbizi katika viunga vya Tripoli halikuwa la kawaida na shambulizi hilo lilifanywa na ndege ya Umoja wa Falme za Kiarabu aina ya F-16. Amesema, anaamini kuwa kituo kimoja cha jeshi la Misri karibu na fukwe za bahari ya Mediterranean ndicho kilichotumika kufanya shambulizi hilo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages