LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 6, 2019

KIONGOZI WA DAESH (ISIS) ALIYEKUWA AKITOA HUKUMU ZA KIFO, ATIWA MBARONI MOSUL

Kiongozi wa Daesh (ISIS) aliyekuwa akitoa hukumu za kifo, atiwa mbaroni Mosul
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq imetangaza kwamba, kiongozi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) aliyekuwa akihusika kutoa hukumu za kifo, ametiwa mbaroni mjini Mosul.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq, Sa'ad Madani ameshiria pia kutiwa mbaroni kiongozi mwingine wa kundi hilo aliyekuwa akihusika na utekelezaji wa mauaji hayo na kuongeza kuwa, jeshi la polisi la Iraq limemtia mbaroni gaidi huyo katika eneo la Al Qayyarah la mkoa wa Nainawa (Nineveh), mashariki mwa Iraq. Madani ameongeza kuwa gaidi huyo ametiwa mbaroni alipokuwa amejificha kwa kuvalia mavazi ya kike. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq, kiongozi aliyekuwa akiwalazimisha watu kutubu na kutoa hukumu za kifo dhidi yao zilizopelekea kuuawa idadi kubwa ya raia na askari wa serikali ya nchi hiyo, alikuwa mjini Mosul katika kipindi ambacho kundi hilo la ukufurishaji lilikuwa likidhibiti mji huo.
Magaidi wa kundi la Daesh (ISIS) ambao ni zao la Marekani na Saudi Arabia
Aidha Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo amesema kuwa gaidi huyo mwenye asili ya Iraq ametiwa mbaroni katika moja ya majengo yaliyoachwa na wakazi wa kusini mwa Mosul, makao makuu ya mkoa wa Nainawa (Nineveh). Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) liliivamia Iraq mwaka 2014 kwa uungaji mkono wa hali na mali wa Marekani na washirika wake wa Magharibi na Kiarabu sambamba na kuyadhibiti maeneo mapana ya kaskazini na magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu. Katika kipindi hicho kundi hilo lilitekeleza jinai na mauaji makubwa dhidi ya raia na maafisa wa serikali ya Iraq. Hata hivyo jeshi la Iraq kwa msaada wa washauri wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lilifanikiwa kufunga faili la kundi hilo baada ya kudhibiti ngome ya mwisho ya Daesh tarehe 17 Novemba 2017 katika eneo la Rawa, la mkoa wa Al-Anbar.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages