LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 6, 2019

TAMASHA LA 8 LA WAHITIMU WALIOFADHILIWA MASOMO NA YTB LAFANYIKA MJINI ANKARA UTURUKI

YTB.jpg

Tamasha kwa ajili ya wahitimu waliokuwa wakisoma katika vyuo vikuu nchini Uturuki waliodhaminiwa na YTB limefanyika  mjini Ankara Jumatano.
Tamasha hilo limefanyika  katika ukumbi wa chumba cha biashara mjini Ankara.
Wanafunzi waliohitimu  kutoka katika vyuo vikuu vya Uturuki waliokuwa wakidhaminiwa na  taasisi hiyo ya YTB wameonekana kuwa wenye furaha wakati wakikabidhiwa shahada zao.
Rais wa Uturuki  Recep Tayyıp ErdoÄźan ameshiriki katika  tamasha hilo na kuwapongeza wanafunzi.
Waziri wa utamaduni na utalii Mehmet Nuri Ersoy amewapongeza  wanafunzi waliohitimu katika hotuba yake aliotoa katika tamasha hilo.
Wanafunzi 1500 wamehitimu Uturuki mwaka 2019.
Katika hotuba yake waziri wa  utamaduni amekumbusha kuwa wanafunzi waliohitimu wamekuwa wawakilishi wa kauli ambayo hupenda kutumiwa na rais ErdoÄźan kuhusu mataifa matano yenye kura ya turufu  ambayo inafahamika kama « Dunia ni kubwa kuliko mataifa matano »
Miongoni mwa wanafunzi 20 waliofanya vizuri shuleni yumo mwanafunzi kutoka nchini Burundi aliekuwa katika kitivo cha Sayansi ya Jamii kwa jina la Ramadhan Shabani.
Wanafunzi hao wamepongezwa na rais ErdoÄźan pamoja na waziri wa elimu akiwemo pia mkurugenzi wa taasisi ya YTB
Kwa upande wake  mkurugenzi wa YTB Abdullah Eren ameonesha umuhimu wa udhamini  wa masomo Uturuki.

Tagi: Abdullah Eren , ErdoÄźan , Uturuki , YTB

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages