LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 6, 2019

MVUA KUBWA YASABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI NA KUJERUHI WATU WATANO

Mafuriko na maporomoko ya ardhi Japan

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa vimesababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi watu watano kusini magharibi mwa Japan.
Kulingana na shirika habari la Kyodo, maafisa wa uokoaji wa eneo hilo wamethibitisha kuwa jiji la Soo limepoteza mwanamke mwenye umri wa miaka 70 mapema wiki hii kutokana na mvua kubwa katika mkoa wa Kagoshima.
Kwa mujibu wa shirila la habari la NHK, polisi amesema kuwa mwanamke mzee ambaye nyumba yake imeharibiwa na mvua hizo amepoteza maisha katika eneo la Kagoshima.
Mamlaka imesema kwamba maporomoko ya ardhi yamepelekea kujeruhiwa kwa watu watano.
Nyumba 80 zimeangamia huku nyumba takriban 700 zikiwa zimebaki bila umeme.
Waziri Mkuu wa Japan Abe Shinzo, katika taarifa hiyo ameahidi kuwa shuguli za uokoaji zinaendelea.
Shirika la Hali ya Hewa la Japani, limesema kiwango cha mvua kimeanza kupungua, lakini mikoa ya Kagoshima, Miyazaki na Kumamoto yanaendela kukumbwa na maporomoko ya ardhi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages