LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2019

RAIS DK. MAGUFULI AMNG'OA JANUARI MAKAMBA, BASHE ATEULIWA UNAIBU WAZIRI

Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Dk. John Magufuli amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira badala ya January Makamba ambaye uteuzi wake ametengua.

Pia Rais Magufuli amemteua Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo badala Innocent Lugha Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, imesema kadhalika Rais Magufuli amemteua Balozi Dk. Martin Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

"Balozi Dk. Lumbanga ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili na uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 21 Julai, 2019", Imesema, taarifa hiyo ya Ikulu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages