Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge kazi na wenyeulemavu, Stella Ikupa ameitaka Manispaa ya Temeke kutoa mikopo kwa wanawake, Vijana na Walemavu kwa wakati ili makundi hayo ya fanyekazi kazi ya kujiingizia kipato.
Ikupa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wanawake wajasiliamali Yombo Buza na wakati akizungumza ikiwa mgenirasmi katika baraza la Wanawake UWT, Yombo vituka akiwa ameambatana na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dar es salaam Mhe Mariam Kisangi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Temeke Mhe Abdalah Mtolea.
Naibu Waziri huyo alifikia hatua hiyo baada ya akinamama kumweleza kutoridhishwa kwao na kasi na utaratibu wa utoaji mikopo katika Manispaa hiyo ambapo walisema wamekuwa wakisumbuliwa kwa hata baada ya kutimiza masharti ya mikopo hiyo lakini hawajapata.
"Walituambia tujiunge katika vikundi vya watu kumi, tuandike Katiba, yote tumefanya lakini imekuwa danadana nenda rudi, tumetumia pesa lakini hatuoni nilini mikopo hiyo watatoa tumekata tamaa hadi tumeanza kukopa hela za riba kwa Mhindi wengine hapa tumeshaanza chukuliwa hadi vitu vya ndani maana riba ni kubwa ukikopa 100,000 unalipa 150,000 "Alisema Happiness Gomba.
Hata hivyo kufuatia malalamiko hayo Mhe Ikupa alilazimika kupiga simu kwa Afisa Maendeleo Manispaa ya Temeke na Meya wa Manispaa hiyo Abdalah Chaulembo, ili kupata ufafanuzi kuhusu utaratibu wa mikopo hiyo ambapo alisema Manispaa inatoa mikopo kwa Vikundi vya vijana kwa kuwa nunua vifaa vya kuanzisha viwanda vidogo vidogo mfano kiwanda cha matofali, wenye ulemavu wanapewa Bajaji, kwa upande wa vikundi vya wanawake wanapewa mashine za kusaga, na wale wanaotaka kufanya biashara ndogondogo wanapewa pesa kwaajili ya biashara zao.
"Nashukuru nimezungumza nao nanyi mmesikia Meya Kasema pesa zipo watakukopesheni, Afisa Maendeleo amesema mwende ofisini muonane naye, naomba sasa tufungue ukurasa mpya yaliyopita sindwele" Alisema Ikupa.
Pamoja na hayo aliwataka wanawake hao kukisemea mema chama cha Mapinduzi kwa wananchi kwani Serikali ina tekeleza vyema Ilani ya Chama kila mmoja anaona miradi mikubwa ya maendeleo inatekelezwa, Shirika la ndege limefufuliwa, hospitali, barabara vituo vya afya vinajengwa nchinzima.
"Ndugu zangu Rais naye ni Binadamu akifanya mazuri tumpongeze ili tumpe moyo wa kuendelea kupata nguvu ya kufanya kazi ya kutuletea maendeleo" Alisema.
Kwa upande wake Mbunge Mariam Kisangi aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi Katika kugombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa Kufanyika mwakahuu ili kuongeza nafasi za uwakilishi wa wanawake.
Pia aliwataka kuwahamasisha Mabinti ambao wamefikia umri wa kupiga kura kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la wapiga kura pindi litakapo anza kufanyiwa Maboresho.
Naye Mbunge wa Temeke Mhe. Abdalah Mtolea aliwapongeza wabunge wa viti maalum Mkoa wa Dar es salaam kwa kutoa muda wao kuwatembelea akinamama na kusikliza kero zao na kuahidi kushirikiana nao katika Kutatua changamoto zinazowakabili.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇