LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 9, 2019

NAIBU WAZIRI WA AFYA AIPONGEZA MOI KWA KAZI NZURI

 Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameipongeza MOI kwa utoaji wa huduma bobezi za Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo wakati alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika viwanja vya Sabasaba

Naibu Waziri alisema ''Niwapongeze kwa huduma ambazo mnazotoa na kuifanya Tanzania kuwa kati ya nchi 6 pekee Afrika,kufanya upasuaji wa mivunjiko ya nyonga,kiuno na hasa kikombe cha mfupa wa nyonga".

 Mkurugenzi  Mtendaji wa MOI,Dkt Respicius Boniface alisema, Mhe. Naibu Waziri, MOI sasa imebobea katika nyanja ya upasuaji ubongo kwa wagonjwa  wanaovilia damu  kwenye ubongo kwa darubini maalumu (Brain aneursym clipping), ambayo imeanza kufanyika hivi karibuni. 


Dkt William Mgisha ambae ni mmoja wa watoa huduma katika maonesho hayo alisema idadi ya madaktari bingwa wabobezi wa nyonga na kiuno 
 (pelvic acetabular surgeons) imefikia watano (5) na kupelekea kuleta ufanisi wa upasuaji wa eneo hilo muhimu kwa wagonjwa.





Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika picha ya pamoja. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages